Jumatatu, 10 Julai 2017
Jumapili, 1 Januari 2017
SALAMU ZA MWAKA MPYA 2017
GREAT
MESSAGE TO THE SOLIDERS OF JESUS CHRIST AND OTHERS
Please
read it(Somaaaa itakusaidia sana)
UJUMBE
WA MWISHO WA MWAKA 2016 NA MWANZO WA MWAKA 2017
Yaliyomo







UTANGULIZI
Mafanikio
ya mtu hupimwa pale anapoanza au anapomaliza. Akiwa anaanza (MWANZO) basi
hupimwa kwa mikakati yake na maandalizi yake kwajili ya jambo lililopo mbele
yake. Mtu akiwa na maandalizi hafifu basi hata mafanikio yake yanakuwa hafifu
au anapata hasara kabisa kwa jambo analotaka kulifanya. Hivyo kila mtu anapaswa awe mwangalifu wa kila mwanzo wa
chochote. Na kwa upande mwingine mafanikio ya mtu hupimwa kupitia MWISHO WAKE,
mwisho wa kitu chochote ndipo unapima kama mtu amefanikiwa au la! Mikakati yake
na mambo aliyotakiwa kuyafanya je amefanikiwa au la! Katika ujumbe huu wa
mwanzo wa mwaka 2017. Nitazungumzia mambo machache kila mtu anapaswa kuzingatia
kila afikapo mwanzo wa mwaka na mwisho wa mwaka. Barikiwa na ujumbe huu!! Ni vyema kama utautuma na kwa rafiki zako nao
wajifunze mambo haya bado hawajachelewa kufanya kila lililopo humu.
1. MWISHO WA MWAKA
Mfano
juu ya mtazamo wangu juu ya neno “Mwisho wa mwaka”
Mwisho wa mwaka ninaufananisha
na Mwanariadha maarufu awapo uwanjani
katika mashindano ya kukimbia ya mita 10,000; ambapo amekimbia muda mrefu, kwa
nguvu nyingi akiwa na nia ya kumaliza mbio akiwa mshindi. Ambapo anapo karibia
kuufikia mwisho anageuka nyuma na kuangalia kama kuna aliye karibu naye au la!
na hapo ndipo anagundua kwamba hakuna aliye karibu naye, huku anaendelea
kuufikia mwisho anatafakari wale wote alioanza nao mbio wameelekea wapi. Anaamua
kugeuka tena mara hii anawaona wachache tu kwa mbali wanamfuata; hapop teana
anajiuliza, Kwanini ni hawa tu wengine wa wapi? Maswali haya anajiuliza japo
anatamani kuweka rekodi ya kumaliza akiwa mshindi wa kwanza kwa kuwaacha
wenzake umbali mrefu.
Anapoendelea kujiuliza hivyo
anashangaa amekwisha maliza umbali wote aliotakiwa kukimbia, na anashangiliwa
kwa kumaliza mbio zile kwa nafasi ya kwanza. Anajikuta amemaliza yeye peke yake
wa kwanza na wengine wachache wakaja baadae kwa kuchelewa ila wengine walishindwa
kabisa kufika. Ndipo hapo anapata majibu kwamba wengine hawakujiandaa
vyakutosha hivyo milli yao iliishiwa nguvu na wengine miili yao ili kuwa dhaifu
hivyo waliishia katikati pia wengine walikata tamaa baada ya kuona wanapitwa na
wenzao. Kitu kilicho nifurahisha ni
baada ya yule mwana riadha kuona vile
alipiga magoti pale pale uwanjani na kumshukuru Mungu.
Mambo
ya kufanya ifikapo mwisho wa mwaka Kutokana na mfano huo;
Ni wengi ambao tumeanza nao
mwaka 2016 lakini hadi kufikia tarehe 31/12/2016 hatuwaoni, hatupo nao
wamefariki. Wengine mili yao imekuwa ni dhaifu na wamelazwa hospitalini.
Wengine wameondokeawa na wapendwa wao. Pia wengine wameshindwa kumaliza mwaka
wakiwa washindi wa kwanza kama yule mwanariadha, waliweka malengo mengi kwaajili
yam waka 2016 kiuchumi, kielimu na kijamii lakini hawajafanikiwa.
Kitu cha Muhimu cha kujiuliza
ni kwamba wewe ni nani hata umalize mwaka ukiwa mshindi? Kwanini yale yote
uliyoyapanga yamefanikiwa? Je wewe ni bora kuliko wao? Je upo hai kutokana na
matendo yako mema? Jibu la maswali haya na mengine mengi kama haya ni hili “HAPANA”. Sio kwammba wewe
ni mwema sana kuliko wengine au ni bora kuliko wengine ila ni KRISTO aliye
kustahilisha tu. Kwa neema yake nyingi na ya ajabu.
v Mshukuru Mungu kwa kufika mwisho huu salama
haijalishi upo katika hali gani; umgonjwa au umeondokewa na
mpendwa wako. Nimekufananisha na mwana riadha hodari kwasababu ndivyo fikra za
mwanadamu zinavyo mdanganya pale anapoona amevuka mwaka wa kwanza, wa pili hadi
miaka arobaini kwa ushindi hapo hujisahau na kushindwa kumtukuza Mungu kwa
kumfikisha mwaka mwengine. Mwanariadha yule mahiri wa kushindana alipofika
mwisho alitafakari na kujiona kwamba sio kwa uwzo wake ila ni kwa neema ya
Mungu tu, alipiga magoti na kumtukuza Mungu. Ndivyo unavyopaswa ufanye mpendwa
mshukuru Mungu kwa maana ni kwa neema yake kuu amekupa uhai na amekushindia
majaeibu mbalimbali uliyopitia.
v Kiri/Yaseme mbele za Mungu, kwa kinywa
chako yale yote Mungu aliyokutendea. Yataje yote unayoyakumbuka
makubwa kwa madogo na yale usiyo yakumbuka yataje kwa ujumla wake ukisema neno
hili “PAMOJA NA YALE NISIYO YA FAHAMU. Kitendo cha kuyakiri mojamoja kila jambo
ambalo Mungu amekutendea kwa kipindi cha mwaka mzima, tabia hii inamfurahisha
Mungu na inaonyesha kwamba unathamini yale ambayo MUNGU amekutendea. Mfano wa kutaja ni huu: Na kushukuru
Mwenyezi Mungu kwa jinsi ulivyonipigania katika mwaka mzima huu umenipa elimu
na umenipandisha kwenye viwango vya juu vya grade A uhimidiwe Bwana. Pia huku
nipungukia umenipa kazi nzuri nitakayopata mshahara mzuri…… Huu ndiyo wakati ambao Mungu anatulia na
kusikiliza shukrani zako na anajivunia kwa yale yote aliyokutendea. Faida ya
kuomba hivi ni hii; 1Unaonyesha
unyenyekevu mbele za Mungu hivyo Mungu atakuinua Zaidi katika mwaka mpya. 2Unaonyesha
kwamba umethamini kile Mungu alicho kutendea hivyo atatenda Zaidi. 3Mungu
atakupa upendeleo wa baadhi ya mambo ambayo yanapaswa yatendewe kazi ili ufalme
wake uinuliwe. 4Mungu atakupa hata vile ambavyo huja mwomba. Faida
zipo nyingi sana iliyokuu ni kwamba Mungu atakupenda Zaidi na Zaidi na
atatamani kukusaidia kila wakati na kukuinua. Soma Zab. 34:7-9, 125:1-2
2. MWANZO WA MWAKA
MAMBO
YA KUZINGATIA UNAPOUANZA MWAKA
Kuanzia Mita 1 hadi mita 10000 kwenye
riadha huu ni umbali wa mwaka mzima: mwaka una miezi kumi na miwili ambapo ni
siku 365. Ndani ya mwaka mzima huu kuna kukata tamaa kutokana na yale
uliyoyategemea hayajafanikiwa au kile ulicho kipanga hakijafanikiwa au
hujajiandaa vyema.
Kabla ya mwaka haujaisha
unapaswa kuzingatia haya: 1Mshukuru
Mungu kwa mwaka unaoisha, kama nilivozungumza hapo juu kwamba kufanya hivi
kunaushusha uwepo wa Mungu lakini kunamweka Mungu tayari kwaajili ya kukusaidia
pindi tu mwaka mpya unapoanza, 2Kamata
siku, masaa, dakika, na sekunde katika maombi; Huku kutakuhakikishia ulinzi muda wowote
kwenye ya mwaka unaoanza ukiwa umelala au upo macho Malaika wa Bwana watakuwa
na wewe (Zab.34:7). 3Weka mikakati kwaajili ya
mwaka mzima na mshirikishe Mungu
mikakati hiyo. Jambo hili litakupa uwezo wa kuwa na nidhamu ya muda na
nafasi utakazozipata tokea mwanzo hadi mwisho wa mwaka, hutatamani muda upotee.
Pia kumshirikisha Mungu mikakati yako ni
kumshirikisha Mungu maisha yako na Mungu akihusika kwenye maisha yako yote basi
ushindi ni lazima. Kila wakati utakapoenda mbele za Mungu katika kipindi cha
mwaka mzima ukiwa unaomba kwaajili yako utamkumbusha malengo haya na mengine
atakayokuonyesha, Pia utaishi kwa malengo ya kufika sehemu fulani kila iitwapo
leo, na malengo yako utafanya juhudi kuyatimiza. 4. Kiri ushindi juu ya mwaka huu mpya, Yoh 1 inatuambia
kuhusu Neno kufanyika mwili, ndivyo ilivyo Mungu alitamka kwenye uumbaji ikawa
, katika uumbaji wote alisema Maneno haya “NA IWE….” “Ikwa” (Mwa.1). Nasi
tuliumbwa kwa mfano wa Mungu hivyo tumepewa uwezo wa kuumba kupitia vinywa
vyetu, Neno linasema Uzima na Mauti vipo katika uwezo wa Ulimi. Hii ndivyo
ilivyo , ndiyo maana tunaona mzazi anaweza kumlaani mtoto na ikawa. Na si hivyo
tuu bali unaweza kujitamkia jambo baya nalo likatokea basi kama ni hivyo
unapoingia kwenye mwaka mpya tarehe za kwanza unaanza kuutamkia Baraka na
mafanikio mwaka huo juu yako na kwa ndugu zako hata majirani na taifa kwa
ujumla.
NAKUTAKIA HERI YA MWAKA
MPYA!!!!!!! MWAKA HUU UKAWE WA BARAKA TELE MAISHANI MWAKO NA WENYE MAFANIKIO
TELE. AMEN;
BY PRIEST MELCHIZEDEK POKEAELI!!!!!!(C) Jan.-2016 pokeaeli
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)