Leo tarehe 26.10.2018 siku ya kwanza ya Semina tutaangalia vipengele viwili wa kwanza vya somo letu la *SIKU NA NYAKATI ZA MWISHO*
Tunaenda kutazama *``` DALILI ZA SIKU ZA MWISHO```* na kuhusu *``` MPINGA KRISTO NA KAZI ZAKE```*
Tuanze na kuhusu *DALILI ZA SIKU ZA MWISHO*
Zipo dalili nyingi sana zilizotabiriwa kwenye Biblia kuhusu siku za mwisho nazo ni hizi kulingana na zilivyoainishwa katika Biblia
Utapitia kwa karibu ukipata muda kitabu cha Mathayo 24, Marko 13, Daniel 12:1-5, 2 Timotheo 3:1-8
Tuziangalie kwa uchache dalili zenyewe
*KUWEPO KWA MAKRISTO WA UONGO:* Naamini wote tumewasikia watu wakijiita Yesu na hata kutenda miujiza na kudanganya wengi wametokea baadhi kule Brazil na Russia tena huyu wa Russia ameoa na ana watoto na bado anajiita Yesu na kujipatia wafuasi wengi kwa miujiza yake ya uongo _ Mathayo 24:5_
*KUWEPO KWA VITA NA MATETESI YA VITA NA MCHAFUKO WA AMANI:* Tumezisikia zote vita mbalimbali toka vita ya kwanza ya dunia, na itakuja kuzuka vita ya tatu ya dunia itaangamiza wengi ila Yesu amesema MSITISHWE ULE MWISHO BADO (Nitaelezea hapo mbele kwanini akasema hata vita zikitokea mwisho bado) _ Mathayo 24:6,7_
*MATETEMEKO YA ARDHI NA JUA KUTIWA GIZA (YAANI KUPATWA KWA JUA NA MWEZI__ Lunar & Solar Eclipse):* Ndio hii ni dalili mojawapo ya mwisho wa Dunia, tumeshuhudia matetemeko na matukio ya kupatwa kwa jua hili limetabiriwa pia kama dalili ya kuwa-alert watu kuwa kuja kwa Yesu kumekaribia _ Marko 13:8, Mhubiri 12:1,2_
*MANABII WA UONGO:* Sio tu hao bali hata mitume wa Uongo na waalimu wa uongo watawadanganya wengi sana YAMKINI HATA WALIO WATEULE, watawavuta watu kwa miujiza yao hata kuwageuza imani wasimtumikie Yesu wa kweli omba usiwe miongoni mwa wataodanganywa linda sana IMANI na MOYO wako. _Mathayo 24:12, Ufunuo 2:2_
*UNYAKUO:* Kwa kiingereza wanaiita RAPTURE, maandiko yanasema kuwa itafikia wakati watu wataanza kupotea kwasababu watachukuliwa na Mungu kwenda mbinguni kuepushwa na dhiki za dunia hii. Kama Eliya na Henoko walivyonyakuliwa itatokea hivyo kwa watu wa Mungu hivi punde. Watakaa watu wawili mmoja atatwaliwa na mmoja ataachwa. Omba usiachwe mpendwa. _Mathayo 24:40,41_
*KUHUBIRIWA INJILI YA KRISTO KWA ULIMWENGU WOTE:* Niwadokezee siri hapa, mpaka leo Yesu hajarudi SABABU kubwa ni kwakuwa _bado injili haijahubiriwa kwa mataifa yote_ Injili ikishafikia kila kiumbe ndipo na yeye atakapokuja. Hataki ukose mbingu kwa kisingizio kuwa hukuisikia Injili. Hivyo usishangae ukiona kasi ya Injili kusambaa ni kubwa ni kwasababu Yesu anataka kurudi. Na jinsi tunavoongeza spidi ya kusambaza Injili ndivyo tunavyoongeza spidi ya Yesu kurudi tena! _Mathayo 24: 14_
*KUJA KWA MPINGA KRISTO AMBAYE NI MTAWALA MKUBWA WA MWISHO DUNIANI ATAKAYEANGUSHWA NA YESU KRISTO ALIYE HAI:*
Kuhusu habari ya Mpinga Kristo ni pana ambayo nimeiandalia makala yake. Tuendelee kuwa pamoja. Nitawaletea hapa hapa.
*USICHOKE TWENDE PAMOJA, KWA MASWALI, MAONI NA USHAURI AU NYONGEZA KARIBU*
Mbarikiwe mno
*_ HUMPHREY MREMA_*