MUNGU ANAKUHITAJI: ENENDA KWA UWEZO ULIO NAO. (Soma Hadi Mwisho hutajuta fuatilia kila siku mwendelezo)
Mungu alipomwita Daudi sio kwamba hakuona kwamba ni Mdogo, au kwamba kwao alikua anadharaulika Ndie wakwenda kuchunga Kondoo za Baba yake.
Waefeso 3:20-21 SUV
"Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu; naam, atukuzwe katika Kanisa na katika Kristo Yesu hata vizazi vyote vya milele na milele. Amina."
Mungu amepanda nguvu ya ajabu ndani yako ya kuwezesha kutoka katika hali uliyo nayo. Kuvuka ng'ambo nyingine. Nguvu ya kuwezesha kufanya mambo makubwa kwenye maisha yako na ukaleta mabadiliko makubwa kwako, kwa familia na jamii nzima.
HILA ZA ADUI NA MBINU ZAKE
Adui anachofanya ni kukuambia kwamba huwezi.
Adui anachofanya kingine ni kukuonesha mazingira ya wengine waliothubutu wakashindwa. Anakutengenezea mazingira magumu Ili na wewe ukate tamaa.
USIKUBALI MAZINGIRA YAKUKWAMISHE
Umaskini usikukwamishe. Kuzaliwa maskini sio makosa yako, makosa yako ni kufa maskini.
KUA NA UJASIRI KAMA WA DAUDI: KUA NA IMANI THABITI KWA MUNGU WETU.
1 Samweli 17:45
"Ndipo Daudi akamwambia yule Mfilisti, Wewe unanijia mimi na upanga, na fumo, na mkuki, bali mimi ninakujia wewe kwa jina la BWANA wa majeshi, Mungu wa majeshi ya Israeli uliowatukana."
Tunalo Jina Lenye Nguvu kupita yote. Kupita Majeshi, Silaha ,Upanga, Njaa Dhiki nk.
INUKA EWE SHUJAA. USISITESITE SONGA MBELE
Ebr 10:38 SUV
"Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani; Naye akisita-sita, roho yangu haina furaha naye."
Waefeso 3:20-21 SUV
"Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu; naam, atukuzwe katika Kanisa na katika Kristo Yesu hata vizazi vyote vya milele na milele. Amina."
Endelea kufuatilia sehemu inayokuja........
@ Rev.Johnson Pokeaeli
Joyful House In Jesus Christ