Isaya 37:30
``[30]Na kwako wewe dalili ndiyo hii; mwaka huu mtakula vitu vimeavyo vyenyewe; na mwaka wa pili mtakula mazao ya mbegu za vitu hivyo; na mwaka wa tatu pandeni mbegu, kavuneni; mkapande mizabibu katika mashamba, mkale matunda yake``
MUNGU NDIYE MPAJI WA MBEGU NA CHAKULA.
- Tunapata mbegu na chakula kutoka kwa Mungu:Mungu ndiye mpaji wa Mbegu+chakula (mavuno)
- Mbegu na chakula ni kanuni ya kimbingu huwezi enda nje na mfumo huo wa kimbingu
Mwanzo 1:12
[12]Nchi ikatoa majani, mche utoao mbegu kwa jinsi yake, na mti uzaao matunda, ambao mbegu zake zimo ndani yake, kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.
Isaya 55:10
[10]Maana kama vile mvua ishukavyo, na theluji, kutoka mbinguni, wala hairudi huko; bali huinywesha ardhi, na kuizalisha na kuichipuza, ikampa mtu apandaye mbegu, na mtu alaye chakula;
2Kor 9:10 SUV
[10] Na yeye ampaye mbegu mwenye kupanda, na mkate uwe chakula, atawapa mbegu za kupanda na kuzizidisha, naye atayaongeza mazao ya haki yenu
- Ili matokeo yaje humwitaji mpandaji na Mungu atoae mvua
Mwanzo 2:5
[5]hapakuwa na mche wa kondeni bado, wala mboga ya kondeni haijachipuka bado, kwa maana BWANA Mungu hajainyeshea nchi mvua, wala hapana mtu wa kuilima ardhi;
Mwanzo 1:12
[12]Nchi ikatoa majani, mche utoao mbegu kwa jinsi yake, na mti uzaao matunda, ambao mbegu zake zimo ndani yake, kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.
Mwanzo 5:3
[3]Adamu akaishi miaka mia na thelathini, akazaa mwana kwa sura yake, kwa mfano wake, akamwita jina lake Sethi.
-seth ni Mbegu toka kwa Mungu
-Nuhu ni Mbegu.
Mwanzo 7:3
[3]Tena katika ndege wa angani saba saba, mume na mke; ili kuhifadhi hai mbegu juu ya uso wa nchi yote.
Fuatilia mwendelezo wa somo........
Mwandishi
Rev. Johnson Pokeaeli