Jumapili, 1 Januari 2017
SALAMU ZA MWAKA MPYA 2017
GREAT
MESSAGE TO THE SOLIDERS OF JESUS CHRIST AND OTHERS
Please
read it(Somaaaa itakusaidia sana)
UJUMBE
WA MWISHO WA MWAKA 2016 NA MWANZO WA MWAKA 2017
Yaliyomo
UTANGULIZI
Mafanikio
ya mtu hupimwa pale anapoanza au anapomaliza. Akiwa anaanza (MWANZO) basi
hupimwa kwa mikakati yake na maandalizi yake kwajili ya jambo lililopo mbele
yake. Mtu akiwa na maandalizi hafifu basi hata mafanikio yake yanakuwa hafifu
au anapata hasara kabisa kwa jambo analotaka kulifanya. Hivyo kila mtu anapaswa awe mwangalifu wa kila mwanzo wa
chochote. Na kwa upande mwingine mafanikio ya mtu hupimwa kupitia MWISHO WAKE,
mwisho wa kitu chochote ndipo unapima kama mtu amefanikiwa au la! Mikakati yake
na mambo aliyotakiwa kuyafanya je amefanikiwa au la! Katika ujumbe huu wa
mwanzo wa mwaka 2017. Nitazungumzia mambo machache kila mtu anapaswa kuzingatia
kila afikapo mwanzo wa mwaka na mwisho wa mwaka. Barikiwa na ujumbe huu!! Ni vyema kama utautuma na kwa rafiki zako nao
wajifunze mambo haya bado hawajachelewa kufanya kila lililopo humu.
1. MWISHO WA MWAKA
Mfano
juu ya mtazamo wangu juu ya neno “Mwisho wa mwaka”
Mwisho wa mwaka ninaufananisha
na Mwanariadha maarufu awapo uwanjani
katika mashindano ya kukimbia ya mita 10,000; ambapo amekimbia muda mrefu, kwa
nguvu nyingi akiwa na nia ya kumaliza mbio akiwa mshindi. Ambapo anapo karibia
kuufikia mwisho anageuka nyuma na kuangalia kama kuna aliye karibu naye au la!
na hapo ndipo anagundua kwamba hakuna aliye karibu naye, huku anaendelea
kuufikia mwisho anatafakari wale wote alioanza nao mbio wameelekea wapi. Anaamua
kugeuka tena mara hii anawaona wachache tu kwa mbali wanamfuata; hapop teana
anajiuliza, Kwanini ni hawa tu wengine wa wapi? Maswali haya anajiuliza japo
anatamani kuweka rekodi ya kumaliza akiwa mshindi wa kwanza kwa kuwaacha
wenzake umbali mrefu.
Anapoendelea kujiuliza hivyo
anashangaa amekwisha maliza umbali wote aliotakiwa kukimbia, na anashangiliwa
kwa kumaliza mbio zile kwa nafasi ya kwanza. Anajikuta amemaliza yeye peke yake
wa kwanza na wengine wachache wakaja baadae kwa kuchelewa ila wengine walishindwa
kabisa kufika. Ndipo hapo anapata majibu kwamba wengine hawakujiandaa
vyakutosha hivyo milli yao iliishiwa nguvu na wengine miili yao ili kuwa dhaifu
hivyo waliishia katikati pia wengine walikata tamaa baada ya kuona wanapitwa na
wenzao. Kitu kilicho nifurahisha ni
baada ya yule mwana riadha kuona vile
alipiga magoti pale pale uwanjani na kumshukuru Mungu.
Mambo
ya kufanya ifikapo mwisho wa mwaka Kutokana na mfano huo;
Ni wengi ambao tumeanza nao
mwaka 2016 lakini hadi kufikia tarehe 31/12/2016 hatuwaoni, hatupo nao
wamefariki. Wengine mili yao imekuwa ni dhaifu na wamelazwa hospitalini.
Wengine wameondokeawa na wapendwa wao. Pia wengine wameshindwa kumaliza mwaka
wakiwa washindi wa kwanza kama yule mwanariadha, waliweka malengo mengi kwaajili
yam waka 2016 kiuchumi, kielimu na kijamii lakini hawajafanikiwa.
Kitu cha Muhimu cha kujiuliza
ni kwamba wewe ni nani hata umalize mwaka ukiwa mshindi? Kwanini yale yote
uliyoyapanga yamefanikiwa? Je wewe ni bora kuliko wao? Je upo hai kutokana na
matendo yako mema? Jibu la maswali haya na mengine mengi kama haya ni hili “HAPANA”. Sio kwammba wewe
ni mwema sana kuliko wengine au ni bora kuliko wengine ila ni KRISTO aliye
kustahilisha tu. Kwa neema yake nyingi na ya ajabu.
v Mshukuru Mungu kwa kufika mwisho huu salama
haijalishi upo katika hali gani; umgonjwa au umeondokewa na
mpendwa wako. Nimekufananisha na mwana riadha hodari kwasababu ndivyo fikra za
mwanadamu zinavyo mdanganya pale anapoona amevuka mwaka wa kwanza, wa pili hadi
miaka arobaini kwa ushindi hapo hujisahau na kushindwa kumtukuza Mungu kwa
kumfikisha mwaka mwengine. Mwanariadha yule mahiri wa kushindana alipofika
mwisho alitafakari na kujiona kwamba sio kwa uwzo wake ila ni kwa neema ya
Mungu tu, alipiga magoti na kumtukuza Mungu. Ndivyo unavyopaswa ufanye mpendwa
mshukuru Mungu kwa maana ni kwa neema yake kuu amekupa uhai na amekushindia
majaeibu mbalimbali uliyopitia.
v Kiri/Yaseme mbele za Mungu, kwa kinywa
chako yale yote Mungu aliyokutendea. Yataje yote unayoyakumbuka
makubwa kwa madogo na yale usiyo yakumbuka yataje kwa ujumla wake ukisema neno
hili “PAMOJA NA YALE NISIYO YA FAHAMU. Kitendo cha kuyakiri mojamoja kila jambo
ambalo Mungu amekutendea kwa kipindi cha mwaka mzima, tabia hii inamfurahisha
Mungu na inaonyesha kwamba unathamini yale ambayo MUNGU amekutendea. Mfano wa kutaja ni huu: Na kushukuru
Mwenyezi Mungu kwa jinsi ulivyonipigania katika mwaka mzima huu umenipa elimu
na umenipandisha kwenye viwango vya juu vya grade A uhimidiwe Bwana. Pia huku
nipungukia umenipa kazi nzuri nitakayopata mshahara mzuri…… Huu ndiyo wakati ambao Mungu anatulia na
kusikiliza shukrani zako na anajivunia kwa yale yote aliyokutendea. Faida ya
kuomba hivi ni hii; 1Unaonyesha
unyenyekevu mbele za Mungu hivyo Mungu atakuinua Zaidi katika mwaka mpya. 2Unaonyesha
kwamba umethamini kile Mungu alicho kutendea hivyo atatenda Zaidi. 3Mungu
atakupa upendeleo wa baadhi ya mambo ambayo yanapaswa yatendewe kazi ili ufalme
wake uinuliwe. 4Mungu atakupa hata vile ambavyo huja mwomba. Faida
zipo nyingi sana iliyokuu ni kwamba Mungu atakupenda Zaidi na Zaidi na
atatamani kukusaidia kila wakati na kukuinua. Soma Zab. 34:7-9, 125:1-2
2. MWANZO WA MWAKA
MAMBO
YA KUZINGATIA UNAPOUANZA MWAKA
Kuanzia Mita 1 hadi mita 10000 kwenye
riadha huu ni umbali wa mwaka mzima: mwaka una miezi kumi na miwili ambapo ni
siku 365. Ndani ya mwaka mzima huu kuna kukata tamaa kutokana na yale
uliyoyategemea hayajafanikiwa au kile ulicho kipanga hakijafanikiwa au
hujajiandaa vyema.
Kabla ya mwaka haujaisha
unapaswa kuzingatia haya: 1Mshukuru
Mungu kwa mwaka unaoisha, kama nilivozungumza hapo juu kwamba kufanya hivi
kunaushusha uwepo wa Mungu lakini kunamweka Mungu tayari kwaajili ya kukusaidia
pindi tu mwaka mpya unapoanza, 2Kamata
siku, masaa, dakika, na sekunde katika maombi; Huku kutakuhakikishia ulinzi muda wowote
kwenye ya mwaka unaoanza ukiwa umelala au upo macho Malaika wa Bwana watakuwa
na wewe (Zab.34:7). 3Weka mikakati kwaajili ya
mwaka mzima na mshirikishe Mungu
mikakati hiyo. Jambo hili litakupa uwezo wa kuwa na nidhamu ya muda na
nafasi utakazozipata tokea mwanzo hadi mwisho wa mwaka, hutatamani muda upotee.
Pia kumshirikisha Mungu mikakati yako ni
kumshirikisha Mungu maisha yako na Mungu akihusika kwenye maisha yako yote basi
ushindi ni lazima. Kila wakati utakapoenda mbele za Mungu katika kipindi cha
mwaka mzima ukiwa unaomba kwaajili yako utamkumbusha malengo haya na mengine
atakayokuonyesha, Pia utaishi kwa malengo ya kufika sehemu fulani kila iitwapo
leo, na malengo yako utafanya juhudi kuyatimiza. 4. Kiri ushindi juu ya mwaka huu mpya, Yoh 1 inatuambia
kuhusu Neno kufanyika mwili, ndivyo ilivyo Mungu alitamka kwenye uumbaji ikawa
, katika uumbaji wote alisema Maneno haya “NA IWE….” “Ikwa” (Mwa.1). Nasi
tuliumbwa kwa mfano wa Mungu hivyo tumepewa uwezo wa kuumba kupitia vinywa
vyetu, Neno linasema Uzima na Mauti vipo katika uwezo wa Ulimi. Hii ndivyo
ilivyo , ndiyo maana tunaona mzazi anaweza kumlaani mtoto na ikawa. Na si hivyo
tuu bali unaweza kujitamkia jambo baya nalo likatokea basi kama ni hivyo
unapoingia kwenye mwaka mpya tarehe za kwanza unaanza kuutamkia Baraka na
mafanikio mwaka huo juu yako na kwa ndugu zako hata majirani na taifa kwa
ujumla.
NAKUTAKIA HERI YA MWAKA
MPYA!!!!!!! MWAKA HUU UKAWE WA BARAKA TELE MAISHANI MWAKO NA WENYE MAFANIKIO
TELE. AMEN;
BY PRIEST MELCHIZEDEK POKEAELI!!!!!!(C) Jan.-2016 pokeaeli
Alhamisi, 7 Julai 2016
Jumatano, 22 Juni 2016
CHRISTIANS FORUM: THE DUTY OF A WIFE IN CHRISTIAN MARRIAGE
CHRISTIANS FORUM: THE DUTY OF A WIFE IN CHRISTIAN MARRIAGE: GREAT!!!!GREAT!!!!! MESSAGE!!!! THE ONE RESPONSIBLE FOR THE GOOD MARRIAGE IS WIFE. IT IS TIME TO FULFILL YOUR DREAMS OF HAVING THE ...
HAPPINESS IN MERRAGE WIFE IS THE SOURCE.
IT IS TIME TO FULFILL YOUR DREAMS OF HAVING THE HAPPY AND SUCCESSFUL MARRIAGEToday's challenges and pressures can make fulfilling marriage seen like an impossible dream. yet God delights in doing the impossible if only we would ask!wife u have to pray for your husband {to be} concerning these key areas:
- His Spiritual walk
- His Emotions
- His health and physical protection
- His security in work and finances
- His role as a father, leader, and decision -maker.
- His faith and his future
Wake up now women your the source for the development of your marriage Psalm 68:11 "The Lord gave the word: great was the company of those that published it."BE BLESSED By Priest Melchizedek PokeaeliGREAT!!!!GREAT!!!!! MESSAGE!!!! THE ONE RESPONSEBLE FOR THE GOOD MARRIAGE IS WIFE.
THE DUTY OF A WIFE IN CHRISTIAN MARRIAGE
GREAT!!!!GREAT!!!!!
MESSAGE!!!! THE ONE RESPONSIBLE FOR THE GOOD MARRIAGE IS WIFE.
IT IS TIME TO FULFILL YOUR DREAMS OF
HAVING THE HAPPY AND SUCCESSFUL MARRIAGE
Today's challenges and
pressures can make fulfilling marriage seen like an impossible dream. yet God
delights in doing the impossible if only we would ask!
wife u have to pray for your husband
{to be} concerning these key areas:
- His Spiritual walk
- His Emotions
- His health and physical protection
- His security in work and finances
- His role as a father, leader, and decision -maker.
- His faith and his future
Wake up now women your the
source for the development of your marriage Psalm 68:11 "The Lord gave the
word: great was the company of those that published it."
Jumanne, 14 Juni 2016
MAANA YA MAOMBI - MAOMBI, MAOMBI, MAOMBI
MAOMBI: Ni njia pekee aliyopewa Mwanadamu, ambayo kwayo anaweza kuzungumza na Mungu wake na kumweleza lolote naye akamsikiliza. Iwe shukrani au mahitaji yake pia mahitaji ya wengine.
Maombi ni wito; kwa Mkristo kutoka kwa Mungu mwenyewe. Mungu anawaita wakristo kwa jambo maalumu Mungu anataka walitende; kama Mungu anasema katika Neno lake "Niite nami nitakuitikia nami nitakuonyesha mambo makubwa na magumu usiyoyajua" (Yer 33:3). Mungu anatoa wito kwa wanadamu wote kumwita wakati wowote wa shida na wa raha naye Mungu atamwoshesha mambo makubwa na Magumu asiyoyajua. Kunakuitwa na Mungu kwaajili ya mapenzi yake ni kazi ya wanadamu kuitikia sauti ya Mungu. Katika Neno hilo hapo juu Mungu anataka wanadamu wamwite ili awasaidie katika shida walizonazo. Kwa kawaida wanadamu wanakutana na mambo makubwa na magumu katika maisha yao; suluhisho la mambo hayo ni maombi pekee.Mungu pia anamwambia mwanadamu "Njooni kwangu ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo nami nitawapumzisha" (Mathayo 11:28). Masumbuko yote na mizigo yote wanadamu tunayopitia utatuzi wake ni kwenye maombi. Hakuna pengine tunapoweza kupata pumziko zaidi ya kuingia kwenye maombi. Mungu anatuita akisema twende kwake naye atatupumzisha. Tukimbilie kwake naye atatufuta machozi yetu.
Maombi ni njia pekee ya kupeleka haja zetu mbele za Mungu badala ya kuwaambia wanadamu wenzetu. Wanadamu wenzetu tunapowaeleza mambo yetu wanaweza wakatutukana wakatusimanga au kutusema vibaya piaa kutusengenya. Pia msaada wa wanadamu una mwisho na lakini Msaada wa Mungu hauna Mwisho. Mungu anasema "Unikumbushe, na tuhojiane; eleza mambo yako, upate kupewa haki yako.(Isaya 43:26)
UMUHIMU WA MAOMBI:Maombi ni kitu chema katika maisha ya Mkristo. Mkristo unapaswa kudumu wakati wote katika Maombi. Maombi yanatuweka karibu na Mungu wetu kwasababu, wakati wote tunakuwa tunazungumza naye. Mwanadamu bila maombi hawezi kufanikiwa. Mfano mdogo ni Mtoto kwa wazazi wake, mtoto huyu akihitaji kitu kwa wazazi wake ni lazima aombe tena kwa busara ndiyo apate kile anachokiomba. Maombi yanatuwezesha kutenda mambo makubwa ambayo hayawezekani kwa yule asiiyeomba maombi yanarejesha na kuimarisha uhusiano wetu na Mungu kila iitwapo leo. Maombi yanonyesha jinsi tunavyomthamini Mungu aliyetuumba na jinsi tunavyomtegemea yeye tu(Zab.115:1). Maombi yanatuimarisha KIROHO. Musa alipokuwa ametoka katika maombi watu wote waliomwona waliona uso wake unang'aa pia kwa Yesu Kristo vivyo hivyo alipokuwa kwenye maombi alibadilika uso nao ulikuwa unang'aa. Tena Maombi hufariji na kutia moyo na kurejesha matumaini yaliyokuwa yamepotea.
HASARA ZA KUTOKUOMBA: Bila maombi huwezi kufanikiwa katika maisha huwezi kusonga mbele na pia hatua ya kiuchumi uliyo nayo utaiona ipo kawaida ila ni mbinu ya shetani ya kukushambulia usiweze kujua kwamba anakushambulia. Kama ukijua kwamba anakushambulia utaacha kulala utakesha kwaajili ya kuomba. Hutakataa tena maombi wala kuwaona wale wanaoomba kwamba wanapoteza Muda katika maombi ila utatamani na wewe ungekuwa na viwango vya maombi kama vyao pia ungeongeza bidii na kumsihi Roho Mtakatifu akupe uwezo wakuzidi kudumu katika maombi bila kukoma; Kama Neno la Mungu linavyosema "Nimeweka walinzi juu ya kuta zako, Ee Yerusalemu; hawatanyamaza mchana wala usiku; ninyi wenye kumkumbusha Bwana, msiwe na kimya;+ wala msimwache akae kimya, mpaka atakapoufanya imara Yerusalemu, na kuufanya kuwa sifa duniani.+" (Isa 62:6)
Mpendwa somo hili linakuhusu wewe amua sasa na kuendelea kufuatilia blog yangu hii ya CHRISTIANS FORUM. christiansforum1.blogspot.com upate mwendelezo wa somo hili.
cha Muhimu ni kuliweka katika matendo somo hili. BARIKIWA NA BWANA.
By Priest Melchzedek P. Pokeaeli.
contactcts: jonson.mwanga@yahoo.com & johnsonmwanga053@gmail.com
ISAYA 54:17 "KILA SILAHA ITAKAYOFANYIKA JUU YAKO HAITAFANIKIWA NA KILA ULIMI UTAKAOINUKA JUU YAKO KATIKA HUKUMU UTAUHESABU KUWA MKOSA. HUU NDIO URITHI WA WATUMISHI WA BWANA NA HAKI YANGU INAYOTROKA KWANGU, ASEMA BWANA."MUNGU NI MWEMA. YU NAMI.
AMEN
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)






