Ijumaa, 9 Julai 2021

MAHUSIANO NA MUNGU

 πŸ’’JOYFUL HOUSE IN CHRISTπŸ’’


πŸŒ…MAHUSIANO NA MUNGUπŸŒ…


Ni ajabu Ila Ni kweli, hatuwezi kusema tunampenda Mungu Kama tunashindwa kuwapenda wenzetu tunaowaona.


Kristo anatufundisha ,tukitaka kumpenda Mungu hakika tunawajibu wa kuwapenda wenzetu Kama tunavyojipenda wenyewe *Mathayo 22:39* na kuwatendea wengine Kama tunavyopenda kutendewa sisi *Mathayo 7:12*


*Tunawezaje kuwapenda wenzetu?*


1. Kwa kuwahurumia. Katika maisha wenzetu wanapitia shida, mahangaiko kwenye mahusiano, familia ,ndoa. Mm nilie jiran natakiwa kumhurumia na kumsaidia kwa sala, mawazo, faraja na kampani. *Luka 6:36*. Tusiseme muache na akome maana anajidai, hapana. Tunatakiwa tuonyeshe huruma .


2. Kristo anatufundisha tukitaka kuwapenda wenzetu Basi tuwe tunawasamehe. Tuwe na mioyo ya kuwasamehe wenzetu wanapotukosea, na tusiwahukumu au kuwanyima Jambo fulani kisa walitukusea siku fulani. Kristo pamoja na kutendewa mabaya hakika aliendelea kusamehe *Luka 23:34*


3. Tukitaka kuwapenda wenzetu Basi tuwe tunawaombea, sala Ina nguvu. Sala inafika pale ambapo sisi wenyewe kimwili hatuwez fika  . Tuwaombee wenzetu wenye shida, wasio mjua Mungu bado, wanaoishi kwenye dhambi ili Neema ya Mungu iwaguse na wapate kuong'oka na kuishi kadiri ya mapenz ya Mungu.


4. Kristo anatufundisha tukitaka kumfuata lazima tujenge tabia ya kuwa wamisionary, watu wa kuwapelekea Habar Njema wengine. Kwa Karne hii ,njia ya kupeleka Habar Njema imezidi kurahishwa maana Kuna vyombo mbalimbali tunavyoweza kuvitumia kuwafikia wengine hasa mitandao ya kijamii. Tutumie mitandao hii kupeleka Ujumbe wa matumaini, Imani, huruma ,upendo kwa wengine. Tusiishie tu kuweka picha, katuni, bali tuweke ujumbe wa Mungu ili wengi wapate kumjua Mungu.


5. Tukitaka kuwapenda wenzetu basi tuwe tunawasaidia wenzetu wasionacho. Tuweke hata malengo ya kila siku,wiki ,mwezi . Mfano, kila siku nitoe 100, 200, 500 , 1000, chochote nilichobarikiwa nacho kumsaidia asie nacho. Basi hata Kama huna kitu, Basi Neno lako la Faraja latosha kwa mhitaji. 


Mungu atubariki Sana.

@Deusdedith Msungo

©JHC 2021.

EVENING GLORY

 ⛪ *JOYFUL HOUSE IN CHRIST*⛪


*EVENING GLORY*

09/07/2021.

-------------------------

 *Mithali 16:9*

*9 Moyo wa mtu huifikiri njia yake;  Bali Bwana huziongoza hatua zake.*


*TAFAKARI FUPI*

Sasa tuko MUHULA wa pili kukamilisha mwaka nikimaanisha tuko mwezi wa Saba sasa. *Unaendeleaje na mabadiliko hayo na ahadi ulizotoa kwa mwaka 2021?*

*Ni kwa viwango gani hiyo mipango yako imekamilika.?*

Ila  Usikate tamaa au kuyaacha  hayo malengo... hata ikiwa kuna shida na changamoto ya kukaa kwenye mstari kutimiza malengo yako . Lakini, hebu  tukumbuke kwamba BWANA ndiye Aziongozae njia zetu, mwisho wa mawazo yetu ndio mwanzo wa njia zake, na Biblia inatueleza kuwa *Yeye anautangaza mwisho tokea mwanzo* hivyo yeye alishajua hatima ya malengo yako tokea Mwanzoni mwa mwaka huu,hivyo 

Nishauku yangu kuona  tunabaki ndani ya kusudi la Mungu, na kumuuliza Bwana Ni wapi anataka tuende na kile anataka tufanye, kisha tuende huko na tufanye.


Then *utakusudia Jambo nalo litathibitika kwako* 


*TUOMBE*

Mungu Mtakatifu, Bwana Mwenyezi, Abba yaan Baba, asante kwa kuwa Ni wa  kushangaza, mtakatifu, na mwenye nguvu. Asante pia kwa kujali kutujali , maisha yetu, maamuzi yetu, na mapambano yetu. Tunaomba tuongoze kwa Roho wako ili tuweze kuelewa Neno lako na kutambua mapenzi yako kwa maisha yetu.ili tukazidi kukuelekezea kikamilifu hatua zetu. Kwa jina la Yesu Kristo ninaomba na kuamini . AMINA


*Nikutakie jioni njema na usiku mwema mpendwa*


*@Dr Mwanga*


*Thus far as God helped us*


*@2021 Joyful house in Christ*

Alhamisi, 8 Julai 2021

MORNING GLORY

 ⛪⛪ *JOYFUL HOUSE IN CHRIST* ⛪

   *MORNING GLORY*

Tar. 09/07/2021.

--------------------------

*Mithali 10:11*

*11 Kinywa chake mwenye haki ni chemchemi ya uzima;  Bali jeuri hufunika kinywa chake mtu mwovu,*

 

=>Ukitaka kujua tofauti kati ya mtu mwadilifu na mtu mwovu? Rahisi, angalia matunda ya maisha yao. Moja ya aina ya matunda inayoonekana katika maisha ya mtu ni *hotuba yake*. Mtu mwadilifu huongea maneno ya hekima, mazuri ambayo ndani yake Kuna *faraja*, uponyaji na Zaidi ya yote uzima 

 *Zekaria 1:13*

*"Naye BWANA akamjibu yule malaika aliyesema nami kwa maneno mazuri, maneno yenye* *faraja.* "

Biblia inasema Wafalme kutoka nchi mbalimbali walimuendea mfalme Sulemani ili kusikiliza Hekima yake. Hii inaonyesha ndani ya hekima ya *Sulemani* walipata suluhisho la changamoto wanazokutana nazo ,na pengine walipata hata miongozo kadhaa ya namna ya kuoongoza nchi zao, Nani anajua! 

Bali Waovu watajidhihirisha kila wakati kwa kile kinywa chake kinasema.kwa sababu ndicho kilichomjaza moyo wake. Mungu ana maana kubwa kutuonya tusikae barazani pa wenye mizaha, tafsiri yake Ni kwamba  hutapata hekima Bali mizaha tu na jeuri. Na mwisho utaishia KUTENDA dhambi.

Zaidi ya yote Mungu anatupenda Sana na ndio maana leo anatukumbusha *1Timotheo 4 :12*

 *Mtu awaye yote asiudharau ujana wako, bali uwe kielelezo kwao waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi* 

=> Ni ombi langu Asubuhi ya Leo ukawe na usemi mzuri wenye Hekima ndani yake ili mtu awaye yote asikudharau daima.


*TUOMBE*

*Tunakushukuru Mungu kwa namna ulivyotuamsha wenye nguvu na afya tele  na kutupa tafakari hii fupi ya neno lako kwa Asubuhi hii  ya leo tunaomba  Maneno ya Vinywa vyetu na tafakari za mioyo yetu na zipendeze mbele zako, Ee Mungu Baba yetu,  mkombozi, na BWANA Wetu ili tukawe vielelezo Bora kwa wale watuzungukao  Sasa na hata milele. Kwa jina la Yesu Kristo Nimeomba na kuamini  Amina.*


Uwe na siku njema!!


@ *Dr Mwanga.*

*Thus far as God helped us*


*@2021 JOYFUL HOUSE IN CHRIST*

Jumanne, 15 Septemba 2020

UWAKILI WETU KWA BWANA

 πŸ’’πŸ’’πŸ™ *JOYFUL HOUSE IN CHRIST*πŸ™πŸ’’ *Morning Glory*πŸŒ„πŸŒ„πŸŒ„πŸŒ„

_16th Sept 2020_

_________________________________


*Somo la Wiki:* UWAKILI WETU KWA BWANA


*MK.12:41-44*

_41 Naye akaketi kulielekea sanduku la hazina, akatazama jinsi mkutano watiavyo mapesa katika sanduku. Matajiri wengi wakatia mengi. 42 Akaja mwanamke mmoja, mjane, maskini, akatia senti mbili, kiasi cha nusu pesa. 43 Akawaita wanafunzi wake, akawaambia, Amin, nawaambia, Huyu mjane maskini ametia zaidi kuliko wote wanaotia katika sanduku la hazina;44 maana hao wote walitia baadhi ya mali iliyowazidi; bali huyu katika umaskini wake ametia vyote alivyokuwa navyo, ndiyo riziki yake yote pia."_


*Mambo ya Kujifunza:*

Utoaji wenye baraka Ni ule unaogusa moyo wa Mungu. Kwa kutoa Katika kweli Yote .

πŸ™πŸŒ„

_Rev.J. Pokeaeli_

πŸ’’

©Sep.2020 Joyful House in Christ

Alhamisi, 16 Januari 2020

PASTORAL ORDINATION (UBARIKIO WA WACHUNGAJI)

Tarehe 1/12/2019 Mchungaji Johnson Paul Pokeaeli Mwanga. Alibarikiwa rasmi kua Mchungaji. Akiwa pamoja na wenzake 23. Siku hiyo walibarikiwa Wachungaji 24 wote wote wa Dayosisi ya Kaskazini Mashariki - Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania.
Ibada hiyo ilifanyikia Usharika wa Kanisa kuu Lushoto Tanga Tanzania(Cathedral)

Mchungaji Johnson ndiye mwanzilishi na mwendeshaji wa Blog hii. Mungu amtunze na kumlinda katika huduma yake na utume huu alioitiwa Amen.


Jumatano, 9 Januari 2019

KITABU CHA MWANZO SURA YA 17-18

[1/9, 10:57] JHC: πŸ€πŸ™πŸΌ *KITABU CHA MWANZO SURA YA 17 -18*πŸ’’πŸ€

πŸ“–†
*SURA YA 1⃣7⃣*

1 Abramu alipokuwa mtu wa miaka tisini na kenda, BWANA akamtokea Abramu, akamwambia, Mimi ni Mungu Mwenyezi, uende mbele yangu, ukawe mkamilifu.
2 Nami nitafanya agano langu kati ya mimi na wewe, nami nitakuzidisha sana sana.
3 Abramu akaanguka kifudifudi. Mungu akamwambia, akasema,
4 Mimi, agano langu nimefanya nawe, nawe utakuwa baba wa mataifa mengi,
5 wala jina lako hutaitwa tena Abramu, lakini jina lako litakuwa Ibrahimu, kwani nimekuweka uwe baba wa mataifa mengi.
6 Nitakufanya uwe na uzao mwingi sana, nami nitakufanya kuwa mataifa, na wafalme watatoka kwako.
7 Agano langu nitalifanya imara kati ya mimi na wewe, na uzao wako baada yako, na vizazi vyao, kuwa agano la milele, kwamba nitakuwa Mungu kwako na kwa uzao wako baada yako.
8 Nami nitakupa wewe na uzao wako baada yako nchi hii unayoikaa ugeni, nchi yote ya Kanaani, kuwa milki ya milele; nami nitakuwa Mungu wao.
9 Mungu akamwambia Ibrahimu, Nawe ulishike agano langu, wewe na uzao wako kwa vizazi vyao baada yako.
10 Hili ndilo agano langu utakalolishika, kati ya mimi na wewe, na uzao wako baada yako, Kila mwanamume wa kwenu atatahiriwa.
11 Mtatahiriwa nyama ya magovi yenu, na jambo hilo litakuwa ishara ya agano kati ya mimi na ninyi.
12 Mtoto wa siku nane atatahiriwa kwenu, kila mwanamume katika vizazi vyenu, mzaliwa nyumbani, na mnunuliwa kwa fedha, kila mgeni asiyekuwa wa uzao wako.
13 Mzaliwa nyumbani mwako, na mnunuliwa kwa fedha yako, lazima atahiriwe; na agano langu litakuwa katika mwili wenu, kuwa agano la milele.
14 Na mwanamume mwenye govi asiyetahiriwa nyama ya govi lake, mtu yule atatengwa na watu wake; amelivunja agano langu.
15 Mungu akamwambia Ibrahimu, Sarai mkeo, hutamwita jina lake Sarai, kwa kuwa jina lake litakuwa Sara.
16 Nami nitambariki, na tena nitakupa mwana kwake, naam, nitambariki, naye atakuwa mama wa mataifa, na wafalme wa kabila za watu watatoka kwake.
17 Ndipo Ibrahimu akaanguka kifudifudi akacheka, akasema moyoni, Je! Mtu wa umri wa miaka mia, kwake atazaliwa mtoto? Naye Sara mwenye umri wa miaka tisini atazaa?
18 Ibrahimu akamwambia Mungu, Lau kwamba Ishmaeli angeishi mbele yako.
19 Mungu akasema, Sivyo, lakini Sara mkeo atakuzalia mwana wa kiume, nawe utamwita jina lake Isaka. Nami nitafanya agano langu imara kwake kuwa agano la milele kwa ajili ya uzao wake baada yake.
20 Na kwa habari za Ishmaeli nimekusikia, nimembariki, nitamzidisha, nami nitamwongeza sana sana. Atazaa maseyidi kumi na wawili, nami nitamfanya awe taifa kuu.
21 Bali agano langu nitalifanya imara kwa Isaka, ambaye Sara atakuzalia majira kama haya mwaka ujao.
22 Mungu akaacha kusema naye, akapanda kutoka kwa Ibrahimu.
23 Ibrahimu akamtwaa Ishmaeli mwanawe, na wote waliozaliwa nyumbani mwake, na wote walionunuliwa kwa fedha yake, wanaume wote wa watu wa nyumba ya Ibrahimu, akawatahiri nyama ya magovi yao siku ile ile, kama Mungu alivyomwambia.
24 Naye Ibrahimu alikuwa mwenye umri wa miaka tisini na kenda alipotahiriwa nyama ya govi lake.
25 Na Ishmaeli mwanawe alikuwa mtu wa miaka kumi na mitatu, alipotahiriwa nyama ya govi lake.
26 Siku ile ile akatahiriwa Ibrahimu na Ishmaeli mwanawe.
27 Na watu wote wa nyumba yake, wazaliwa nyumbani, na wanunuliwa kwa fedha katika mkono wa mgeni, wakatahiriwa pamoja naye.
πŸ“–
*SURA YA 1⃣8⃣*

1 BWANA akamtokea Ibrahimu karibu na mialoni ya Mamre, alipokuwa ameketi mlangoni pa hema yake mchana wakati wa hari.
2 Akainua macho yake akaona, na tazama, watu watatu wamesimama mbele yake. Naye alipowaona alipiga mbio kuwalaki kutoka mlangoni pa hema, akainama mpaka nchi,
3 akasema, Bwana wangu, kama nimeona fadhili machoni pako nakuomba usinipite sasa mimi mtumwa wako.
4 Na yaletwe basi maji kidogo mkanawe miguu, mkapumzike chini ya mti huu.
5 Nami nitaleta chakula kidogo, mkaburudishe moyo, baadaye mwendelee, iwapo mmemjia mtumwa wenu. Wakasema, Haya, fanya kama ulivyosema.
6 Basi Ibrahimu akaenda hima hemani kwa Sara, akasema, Himiza vipimo vitatu vya unga safi, uukande, ufanye mikate.
7 Ibrahimu akapiga mbio kwenda kundini, akaleta ndama wa ng’ombe aliye laini, mzuri, akampa mtumishi, naye akahimiza kuiandaa.
8 Akatwaa siagi na maziwa, na ndama aliyoiandaa, akawaandikia mbele yao, akasimama karibu nao chini ya mti, nao wakala.
9 Wakamwambia, Yu wapi Sara mkeo? Akasema, Yumo hemani.
10 Akamwambia, Hakika nitakurudia wakati huu huu mwakani, na tazama, Sara mkeo atapata mwana wa kiume. Sara akasikia mlangoni pa hema iliyokuwapo nyuma yake.
11 Basi Ibrahimu na Sara walikuwa wazee, na umri wao mkubwa, na Sara alikuwa amekoma katika desturi ya wanawake.
12 Kwa hiyo Sara akacheka moyoni mwake, akisema, Niwapo mkongwe, nitapata furaha, na bwana wangu mzee?
13 BWANA akamwambia Ibrahimu, Mbona Sara amecheka akisema, Mimi kweli nitazaa mwana, nami ni mzee?
14 Kuna neno gani lililo gumu la kumshinda BWANA? Kwa muhula wake nitakurudia, wakati huu huu mwakani, na Sara atapata mwana wa kiume.
15 Akakana Sara, akisema, Sikucheka, maana aliogopa. Naye akasema, Sivyo, umecheka.
16 Kisha watu hao wakaondoka huko wakaelekeza nyuso zao Sodoma. Ibrahimu akaenda pamoja nao awasindikize.
17 BWANA akanena, Je! Nimfiche Ibrahimu jambo nilifanyalo,
18 akiwa Ibrahimu atakuwa taifa kuu, hodari, na katika yeye mataifa yote ya dunia watabarikiwa?
19 Kwa maana nimemjua ya kwamba atawaamuru wanawe, na nyumba yake baada yake waishike njia ya BWANA, wafanye haki na hukumu, ili kwamba BWANA naye akamtimizie Ibrahimu ahadi zake.
20 BWANA akasema, Kwa kuwa kilio cha Sodoma na Gomora kimezidi, na dhambi zao zimeongezeka sana,
21 basi, nitashuka sasa nione kama wanayotenda ni kiasi cha kilio kilichonijia; na kama sivyo, nitajua.
22 Basi wale watu wakatoka huko wakaelekea Sodoma; lakini Ibrahimu alikuwa akali akisimama mbele za BWANA.
23 Ibrahimu akakaribia, akasema, Je! Utaharibu mwenye haki pamoja na mwovu?
24 Huenda wakawapo wenye haki hamsini katika mji, utaharibu, wala hutauacha mji kwa ajili ya hao hamsini wenye haki waliomo?
25 Hasha usifanye hivyo, ukamwue mwenye haki pamoja na mwovu, mwenye haki awe kama mwovu. Hasha; Mhukumu ulimwengu wote asitende haki?
26 BWANA akasema, Nikiona katika Sodoma wenye haki hamsini mjini, nitapaacha mahali pote kwa ajili yao.
27 Ibrahimu akajibu, akasema, Basi, nimeshika kusema na Bwana, nami ni mavumbi na majivu tu.
28 Huenda wakapunguka watano katika wale hamsini wenye haki, je! Utaharibu mji wote kwa kupungua watano? Akasema, Sitauharibu, nikiona humo arobaini na watano.
29 Akazidi tena kusema naye, akinena, Huenda wakaonekana humo arobaini? Akasema, Sitafanya kwa ajili ya hao arobaini.
30 Akasema, Bwana asiwe na hasira, nami nitasema, Huenda wakaonekana huko thelathini? Akasema, Sitafanya, nikiona humo thelathini.
31 Akasema, Tazama, nimeshika kusema na Bwana, huenda wakaonekana huko ishirini? Akasema, Sitaharibu kwa ajili ya hao ishirini.
32 Akasema, Bwana asiwe na hasira, nami nitasema mara hii tu, Huenda wakaonekana huko kumi? Akasema, Sitaharibu kwa ajili ya hao kumi.
33 Basi BWANA alipokwisha kuzungumza na Ibrahimu, akaenda zake; Ibrahimu naye akarudi mahali pake.

*MUNGU AKUBARIKI*

πŸ’’πŸ“–†
©Jan 2019 Joyful House in Christ
[1/9, 18:12] JHC: Sura hizi Mbili tunaona mbo mengi. Ila tutazame mambo machache ya Muhimu hapa.

1:Bwana Anamwona Abramu Na Sarai mkewe bado hawajakamilika.

Katika Mwaka Wa 99 umri Wa Abram Mungu anamtokea Na Kumwambia Atengeneze, Atubu, ajitakase. _"Mimi ni Mungu Mwenyezi uende Mbele yangu ukawe mkamilifu''_

Tazama Kitu anachofanya Abram ni kwamba anaanguka Kifudifudi yaani ana surrender Kwa Bwana. Anatubu. Na Hapo Mungu anampa Jina jipya Na Anafanya agano naye. Dhambi inaweza Ikawa sababu ya Kuchelewesha Baraka zetu. Japo tunazungumza Na Mungu, Tunaomba lakini Bado Mungu akitutazama Anaona kunasehemu hatujakamilika Bado. Kuna kitu tunapaswa kufanya Ili kuzirithi Baraka lltulizoandikiwa.

2. Yeye Na Mkewe wanapewa majina mapya. Majina ya kuwa hai katika Bwana. Majina yaliyobeba Baraka.  Ibrahimu yaani Baba Wa mataifa mengi. Na Sara yaani Mama Wa Mataifa Na Wafalme watatoka kwake. Kunahaja ya Kutakasa majina Yetu Na Kuyatamkia Baraka. Na kuyatenga Na laana au tabia za Mababu. Majina yanazungumza Maisha yako. Yamebeba hatima ya Maisha yako. Kama unaitwa Sikujua au Unaitwa HUZUNI/ MASUMBUKO  bado ni wakati Wa Kutafakari. Aidha tutaona Vizuri jinsi tunavyoendelea kusoma Biblia jinsi kila Jina lilivyo Na Maana.

3. Ili ahadi ya Mungu itimie Mungu anaweka Vigezo anamwambia kwamba kila mwanamume anapaswa kutahiriwa. Hii ilikuwa Alama ya kutenganisha yupi ni Mwebrania yaani Mbarikiwa Wa Bwana Na yupi siye. Ambaye hakutahiriwa hata kama amezaliwa katika ukoo Wa Ibrahimu hawezi kuzirithi Baraka za Mungu Kwa Ibrahimu. Katika Maisha ya Sasa tunatambuliwa Kwa Ubatizo. Unapobatizwa unafanyika kuwa Mrithi Wa Ufalme Wa Mbinguni.

4. Wakati Wa Bwana ukifika kila Kizuizi hukaa pembeni. Wakati Wa Ibrahimu Na Sara mkewe kupata mtoto ulipofika Vizuizi vyote vilikaa pembeni. Havikuweza tena kuzuia. Hata mawazo Na utaalamu Wa kibinadamu kwamba Sasa Ibrahimu ni Mzee Wa miaka 99 Na Mkewe miaka 90 kwamba ameshakoma hichi hakikuweza kuzuia. Na Mungu akamfurahisha Sara katika wakati Wa uzeeni. Usiumie uaiteseke subiri wakati Wa Mungu mpendwa