💒JOYFUL HOUSE IN CHRIST💒
🌅MAHUSIANO NA MUNGU🌅
Ni ajabu Ila Ni kweli, hatuwezi kusema tunampenda Mungu Kama tunashindwa kuwapenda wenzetu tunaowaona.
Kristo anatufundisha ,tukitaka kumpenda Mungu hakika tunawajibu wa kuwapenda wenzetu Kama tunavyojipenda wenyewe *Mathayo 22:39* na kuwatendea wengine Kama tunavyopenda kutendewa sisi *Mathayo 7:12*
*Tunawezaje kuwapenda wenzetu?*
1. Kwa kuwahurumia. Katika maisha wenzetu wanapitia shida, mahangaiko kwenye mahusiano, familia ,ndoa. Mm nilie jiran natakiwa kumhurumia na kumsaidia kwa sala, mawazo, faraja na kampani. *Luka 6:36*. Tusiseme muache na akome maana anajidai, hapana. Tunatakiwa tuonyeshe huruma .
2. Kristo anatufundisha tukitaka kuwapenda wenzetu Basi tuwe tunawasamehe. Tuwe na mioyo ya kuwasamehe wenzetu wanapotukosea, na tusiwahukumu au kuwanyima Jambo fulani kisa walitukusea siku fulani. Kristo pamoja na kutendewa mabaya hakika aliendelea kusamehe *Luka 23:34*
3. Tukitaka kuwapenda wenzetu Basi tuwe tunawaombea, sala Ina nguvu. Sala inafika pale ambapo sisi wenyewe kimwili hatuwez fika . Tuwaombee wenzetu wenye shida, wasio mjua Mungu bado, wanaoishi kwenye dhambi ili Neema ya Mungu iwaguse na wapate kuong'oka na kuishi kadiri ya mapenz ya Mungu.
4. Kristo anatufundisha tukitaka kumfuata lazima tujenge tabia ya kuwa wamisionary, watu wa kuwapelekea Habar Njema wengine. Kwa Karne hii ,njia ya kupeleka Habar Njema imezidi kurahishwa maana Kuna vyombo mbalimbali tunavyoweza kuvitumia kuwafikia wengine hasa mitandao ya kijamii. Tutumie mitandao hii kupeleka Ujumbe wa matumaini, Imani, huruma ,upendo kwa wengine. Tusiishie tu kuweka picha, katuni, bali tuweke ujumbe wa Mungu ili wengi wapate kumjua Mungu.
5. Tukitaka kuwapenda wenzetu basi tuwe tunawasaidia wenzetu wasionacho. Tuweke hata malengo ya kila siku,wiki ,mwezi . Mfano, kila siku nitoe 100, 200, 500 , 1000, chochote nilichobarikiwa nacho kumsaidia asie nacho. Basi hata Kama huna kitu, Basi Neno lako la Faraja latosha kwa mhitaji.
Mungu atubariki Sana.
@Deusdedith Msungo
©JHC 2021.