Alhamisi, 8 Julai 2021

MORNING GLORY

 ⛪⛪ *JOYFUL HOUSE IN CHRIST* ⛪

   *MORNING GLORY*

Tar. 09/07/2021.

--------------------------

*Mithali 10:11*

*11 Kinywa chake mwenye haki ni chemchemi ya uzima;  Bali jeuri hufunika kinywa chake mtu mwovu,*

 

=>Ukitaka kujua tofauti kati ya mtu mwadilifu na mtu mwovu? Rahisi, angalia matunda ya maisha yao. Moja ya aina ya matunda inayoonekana katika maisha ya mtu ni *hotuba yake*. Mtu mwadilifu huongea maneno ya hekima, mazuri ambayo ndani yake Kuna *faraja*, uponyaji na Zaidi ya yote uzima 

 *Zekaria 1:13*

*"Naye BWANA akamjibu yule malaika aliyesema nami kwa maneno mazuri, maneno yenye* *faraja.* "

Biblia inasema Wafalme kutoka nchi mbalimbali walimuendea mfalme Sulemani ili kusikiliza Hekima yake. Hii inaonyesha ndani ya hekima ya *Sulemani* walipata suluhisho la changamoto wanazokutana nazo ,na pengine walipata hata miongozo kadhaa ya namna ya kuoongoza nchi zao, Nani anajua! 

Bali Waovu watajidhihirisha kila wakati kwa kile kinywa chake kinasema.kwa sababu ndicho kilichomjaza moyo wake. Mungu ana maana kubwa kutuonya tusikae barazani pa wenye mizaha, tafsiri yake Ni kwamba  hutapata hekima Bali mizaha tu na jeuri. Na mwisho utaishia KUTENDA dhambi.

Zaidi ya yote Mungu anatupenda Sana na ndio maana leo anatukumbusha *1Timotheo 4 :12*

 *Mtu awaye yote asiudharau ujana wako, bali uwe kielelezo kwao waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi* 

=> Ni ombi langu Asubuhi ya Leo ukawe na usemi mzuri wenye Hekima ndani yake ili mtu awaye yote asikudharau daima.


*TUOMBE*

*Tunakushukuru Mungu kwa namna ulivyotuamsha wenye nguvu na afya tele  na kutupa tafakari hii fupi ya neno lako kwa Asubuhi hii  ya leo tunaomba  Maneno ya Vinywa vyetu na tafakari za mioyo yetu na zipendeze mbele zako, Ee Mungu Baba yetu,  mkombozi, na BWANA Wetu ili tukawe vielelezo Bora kwa wale watuzungukao  Sasa na hata milele. Kwa jina la Yesu Kristo Nimeomba na kuamini  Amina.*


Uwe na siku njema!!


@ *Dr Mwanga.*

*Thus far as God helped us*


*@2021 JOYFUL HOUSE IN CHRIST*

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni