MAISHA MAZURI NI HAKI YA KILA ALIYEUMBWA NA MUNGU
✍️Rev. Johnson Paul Pokeaeli
MAMBO MAWILI MUHIMU
1. Mungu alimwumba Binadamu siku ya sita baada yakumwandalia kila kitu. Chakula, mahali pazuri pakuishi, mazingira salama nk. Soma Mwanzo 1.
2. Mungu alimpa Mwanadamu maarifa ya kuvitumia, na mamlaka Ya kuvitumia na wajibu wa kuvitunza
UUMBAJI SIKU SITA MAANDALIZI KWAAJILI YA MAISHA MAZURI YA MWANADAMU
Siku ya 1: Mungu aliumba nuru iangaze uso wa dunia na kuwezesha kuwa vipindi vya usiku na mchana.—Mwanzo 1:3-5.
Anga na bahari
Siku ya 2: Mungu aliumba anga, au alitenganisha maji yaliyo chini ya anga na maji yaliyo juu ya anga.—Mwanzo 1:6-8
Nchi kavu na mimea
Siku ya 3: Mungu alitokeza nchi kavu. Aliumba pia mimea.—Mwanzo 1:9-13
Siku ya 5: Mungu aliumba viumbe wa kwenye maji na wanaoruka.—Mwanzo 1:20-23
Siku ya 6: Mungu aliumba wanyama na wanadamu.—Mwanzo 1:24-31. .31.
TAMBUA THAMANI YA DUNIA MUNGU ALIYOKUPA
-uhai ni Fursa Kubwa sana kufanya badiliko katika ulimwengu wa Roho na wa MWILI.
•Mungu alipomwumba Mwanadamu alipomaliza alimpulizia Pumzi hai akawa kiumbe hai.
°ungali unaishi bado una nafasi ya kufanya Jambo chanya kwaajili ya maisha yako ya sasa na hata ya baadae.
°TOBA NA MAISHA SAFI -Inakupa uhakika wa maisha mazuri ya Sasa hata ya baadae
*BIDII BINAFSI - Inakupa nafasi ya kupata Chakula Cha Kila siku.
HIVYO VYOTE MUNGU ALIUMBA SIKU SITA KWAAJILI YAKO MWANADAMU.
WEWE NI WATHAMANI MNO.
MTUKUZE MUNGU
MUNGU HAKUUMBA GHOROFA/MAGARI/NDEGE AU TRENI.
ILA ALIMPA MWANADAMU MAARIFA
MUNGU AKASEMA, NA tumfanye mtu Kwa mfano wetu akatawale_.
WEWE NA MIMI TUMEUMBWA KWA MFANO WA MUNGU
USIJIDHARAU KWA NAMNA YEYOTE ILE
____________________________________________
Mwanzo 1:26
[26]Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.
And God said, Let us make man in our image, after our likeness: and let
Wewe ni mfano wa Mungu. Ni sura ya Mungu.
Umepewa kutawala kwasababu wewe umeumbwa na Mungu Kwa mfano wake na sura yake.
HIVYO NDANI YAKO KUNA NGUVU YA AJABU AMBAYO HUJAWAI ONA.
•Hujajisumbua kutaka kuona ni nini Mungu ameweka kama hazina ndani yako na ndiyo maana umebaki hivyo ulivyo na hata umekata tamaa kabisa ya kuishi. Soma ✍️*
Efe 3:20-21 SUV
"Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu; naam, atukuzwe katika Kanisa na katika Kristo Yesu hata vizazi vyote vya milele na milele. Amina."
![]() |
MIKONO ya mwenye BIDII hutajirisha |
Dunia ya Sasa inashuhudia watu wengi wakikata tamaa ya kuishi ........
Sababu eti wamechoka?????
Eti umaskini???????
Mahusiano????????!
Bado hujaelewa nini Mungu ameweka ndani yako ndiyo maana unafikia uamuzi huo.
Nikutahadharishe TU kwamba pia utadaiwa kingi na Mungu kwasababu pia ameweka vipawa, karama na Huduma nyingi ndani yako . *Hivyo hakuna muda wa kupoteza fanya kazi*
MWISHO
Mwanadamu kwa Maarifa Ngu aliyoweka ndani yake ameweza kufanya haya yote yanayoonekana. Nawe amua sasa kutumia kile Mungu amekupatia kuleta mabadiliko duniani.utajiri ni haki yako.
©2023 Mchungaji Johnson Paul Pokeaeli