Alhamisi, 18 Mei 2023

TAMBUA WAKATI WA KUJILIWA KWAKO vol.2

 BWANA ANAJIBU KWA NAMNA USIYODHANI/NJIA ZAKE HAZICHUNGUZIKI

  • usichoke kua na subira/saburi/uvumilivu.
  • Usikate tamaa 
  • Jenga Imani yako Kwa Mungu
  • Linda Amani yako ya moyo wakati wote 
  • Kua na tumani hatakama hitaji lako limekawia kiasi gani



Mfano wa uvumilivu uliojengeka katika Imani Kwa Mungu
  • Ibrahimu alingoja mtoto Kwa muda wa MIAKA Tisini na Kenda NDIPO MUUJIZA wake unatendeka tena katika mazingira ambayo hakutegemea
Tazama uhitaji wa Ibrahimu: kupata mtoto, tena mrithi.

Mwanzo 15:2-4

"[2]Abramu akasema, Ee Bwana MUNGU, utanipa nini, nami naenda zangu hali sina mtoto, na atakayeimiliki nyumba yangu ni huyu Eliezeri, Mdameski? 

[3]Abramu akasema, Tazama, hukunipa uzao, na mtu aliyezaliwa nyumbani mwangu ndiye mrithi wangu. 

[4]Nalo neno la BWANA likamjia likinena, Huyu hatakurithi, bali atakayetoka katika viuno vyako ndiye atakayekurithi. "

  • Kuna tofauti Kati ya mtoto na mrithi
  • Mungu anamuahidi Abram kwamba atampatia mrithi Toka Tumbo la mke wake wa ndoa .
Mwanzo 15:4. "Nalo neno la BWANA likamjia likinena, Huyu hatakurithi, bali atakayetoka katika viuno vyako ndiye atakayekurithi." 

  • Umri unazidi kwenda na Kwa kigezo hicho Abram anaingia kwenye mtego wa kumkosea Mungu 
  • Shetani anaijaribu Imani yake Kwa kuwadanganya kwamba wanaweza kupata mtoto hata Kwa mjakazi.
  • Wanasahau kwamba wanatafuta mrithi na sio mtoto TU.
Mwanzo 16:1-2
"[1]Basi Sarai mkewe Abramu hakumzalia mwana, naye alikuwa na mjakazi, Mmisri, jina lake Hajiri. 

[2]Sarai akamwambia Abramu, Basi sasa, BWANA amenifunga tumbo nisizae, umwingilie mjakazi wangu labda nitapata uzao kwa yeye. Abramu akaisikiliza sauti ya Sarai. "

  • Kua makini wakati unangojea Baraka zako .
  • Unapongojea MUUJIZA WAKO Adui anaweza kukuletea kila aina ya lugha ,ulagahai Ili kukuyumbisha Imani yako Kwa Mungu usikubali
TENGENEZA NA MUNGU ILI UPOKEE BARAKA ZAKO.
  • MUNGU Anapatiliza maovu yetu hata kizazi baada ya kizazi lakini pia ni mwingi wa rehema akikusamehe atakubariki wewe na kizazi chako chote.
  • Katika wakati wa kungojea ulionao umemkosea nini Mungu : je ulienda Kwa waganga? Au ulizini/ukitoka nje ya ndoa Ii kupata mtoto?
  • Kama ulifanya hivyo inapaswa kutenge eza.
Mwanzo 17:1-3
"1]Abramu alipokuwa mtu wa miaka tisini na kenda, BWANA akamtokea Abramu, akamwambia, Mimi ni Mungu Mwenyezi, uende mbele yangu, ukawe m
kamilifu. 

[2]Nami nitafanya agano langu kati ya mimi na wewe, nami nitakuzidisha sana sana. 

[3]Abramu akaanguka kifudifudi. Mungu akamwambia, akasema," 

SOMO HILI LINAENDELEA .......
Endelea kufuatilia masomo hayayatakujenga KIROHO nawe utavuka hatua Moja kwenda nyingine. Amen
✍️✍️Mchungaji Johnson Pokeaeli




Hakuna maoni:

Chapisha Maoni