MBINU ZA KUSHINDA MAJARIBU/MITIHANI
1. UTULIVU
2.IMANI KWA MUNGU
3. IMANI KATIKA UWEZO WAKO (Unaweza)
4.KUTHUBUTU KUFANYA PASIPO HOFU NA MASHAKA.
WAKATI UNAKUTANA NA MAJARIBU USISAHAU HAYA:
_________________
1.Shetani ni baba wa uongo
•atakuambia huwezi
•Atajaribu kukuonesha wengine walioshindwa Ili ukate tamaa.
2. Usitafute njia fupi au ya haraka haraka ya kutoka kwenye jaribu hilo.
•Njia ni Yesu Kristo pekee
3. Linda sana Amani ya Moyo, (hali yako ya KIROHO isiathirike Kwa namna yeyote Ile)
1 Kor 10:13 SUV
"Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili."
Ebr 10:38 SUV
"Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani; Naye akisita-sita, roho yangu haina furaha naye."
Yakobo 1:5
"Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; *naye atapewa.*"
MAOMBI BILA KUKOMA
1.Hakuna Cha kukufanya usimwombe Mungu,Bali vipo vingi na mambo mengi yanayotufanya twende mbele za Mungu Kwa maombi.
2. Maombi ni Mazungumzo na Mungu wetu
•je unatambua hilo?
•tumepewa fursa ya pekee sana sana kupeleka mahitaji yetu Kwa Mungu.
•pale hali inapozidi kua ngumu ndiyo na maombi yazidi Kwa wingi Kwa Mungu.
Yakobo 1:6-8
"[6]Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yo yote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku.
[7]Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa Bwana.
[8]Mtu wa nia mbili husita-sita katika njia zake zote."
Isaya 62:6 SUV
Nimeweka walinzi juu ya kuta zako, Ee Yerusalemu; hawatanyamaza mchana wala usiku; ninyi wenye kumkumbusha BWANA, msiwe na kimya
Hitimisho.
Kristo amestuachia uhakika wa kushinda vita yeyote Inayotukabili. MBINU hizi zikuongoze kusimama kikamilifu ktk Imani.
Endelea kufuatilia masomo yetu . Ahsante
✍️Rev. Johnson Paul Pokeaeli
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni