SABATO KATIKA AGANO LA KALE
Neno sabato lina maana ya mapumziko au siku ya mapumziko..Asili ys mapumziko (Sabato) hayo tunayapata ktk kitabu cha mwanzo,, Mungu alipomaliza kazi ya uumbaji soma (mwa 2:1-3)
Kwa Mujibu wa mistari huyo 👆 Mungu mwenyewe alipumzika. Alihitaji siku moja ya kustarehe baada ya kazi yake ya uumbaji iliyochukua siku sita. Kutokana na umuhimu wa kupumzika kwake akaitakasa akaitakasa siku hiyo ya saba.....Neno "Takasa " linamaana ya kuweka wakfu au kutenga kwajili ya matumizi matakatifu, yaani matumizi maalumu yaliyokusudiwa na Mungu, au kutengwa kwaajili ya Mungu.
Kutoks 16 23-29. Watu wa Mungu waisrael, waliagizwa kwa mara ya kwanza kupumzika siku ya sabato wakupokuwa ktk bara la Sini, ilikuwa kati ya Elimu na Sinai. Kutokana na manung'uniko yao kwa Musa na kwa Haruni kwa sababu ya njaa, Mungu aliwapa chakula kutika mbinguni kilichoitwa Mana.
Aliwataka wakiokote chakula hicho kilichotoka Mbinguni, kila siku.
Akiwataka wasiwe wanaikota chakula cha zaidi ya siku moja. Aliwaonya wakifanya hivyo, chakula chao kingeoza.
Hapo ndipo pia aliwapa amri wasiokote chakula hicho siku ya Sabato kwa maana nisiku takatifu ya Bwana.
Baada ya muda mfupi baada ya hapo , juu ya mlima wa Sinai, Mungu akampa Musa Amri kumi kwaajili ya wana wa Israel, Ikiwemo Amri ya kuitakasa Sabato. "Ikumbuke siku ya Bwana(sabato) na kuitakasa"
SABATO ILIVYOADHIMISHWA KATIKA AGANO LA KALE.
Siku ya Sabato iliadhimishwa kwa njia mbili katika Agano la Kale
Njia ya kwanza :- ilikuwa kuacha kufanya kazi ili kupumzika (Kut 20:8-11) kazi zilizozuiliwa kufanywa zilikuwa zote , ilikuwa pamoja na kutowasha moto ktk nyumba zao (kut 35:3).
Kukusanya kuni (Hes 15:32). Kubeba mizigo (Yer 17:21) kusafiri (Kut 16:29).
nakufanya biashara(Amo 8:5) .Hii ndio sababu Nehamia aliagiza malango ya Yerusalem yafungwe siku ya Sabato ilikutoruhusu wafanya biashara wa nje kuingia ,wala wale wa ndani kutoka siku hiyo(Neh 10:31, 13:15, 19)
Kutoishika sabato lilikuwa kosa kubwa lililosababisha kuuawa kwa anayeasi soma (Kuto 31:14-15, kuto 35:2)
Njia ya pili:-
Njia ya pili ya kuiadhimisha siku ya sabato ilikuwa ya ibada. Kwakawaida waisrael waliagizwa kutoa sadaka ya kuteketezwa , ambayo ilikuwa mwana kondooo wa mwaka mmoja ,mmoja asubuhi na mwana kondoo mwengine jioni(Hes 28:4)
Aidha kwa siku hiyo waliweka mikate mipya ya mahali patakatifu hekaluni (Law 24:8) mikate hiyo ilikuwa kumi na miwili iliopangwa juu ya meza iloitwa meza ya onyesho. Mikate hiyo ililiwa na makuhani tu,, siku ya sabato, ,matendohayo yalikuwa ya Ibada mbele za Mungu
SABATO KATIKA AGANO JIPYA
👉 Yesu na Sabato:- Yesu alizaliwa chini ya sheria (Gal 4:4). Alizaliwa ktk kipindi ambacho watu wa Mungu walihusiana na Mungu kwa taratibu za Agano la Kale :- wazazi wake walitoa sadaka kama torati ilivyoagiza, alitahiriwa siku ya nane alihudhuria sikukuu zao za kiyahudi, ikiwemo sikukuu ya pasaka,aliabudu ktk sinagogi na ktk hekalu ,alishika Sabato
Leo hii hakuna anayehusiana na Mungu kwa kufuata desturi au taratibu za Agano la kale .Hata wasabato wa leo hawatahiri watoto wao siku ya nane,, hawaendi Yerusalem kuhudhuria sikukuu za kiyahudi ,hawaabudu ktk masinagogi, na hawatoi sadaka za kuteketezwa kama walivyofanya wayahudi, ambao ndio waliokuwa watu wa Mungu ktk Agano la Kale.. Swali ni kwa nini?
Ni kwasababu" Hata ulipowadia utimilifu wa wakati ,Mungu alimtuma mwanae ambaye alizaliwa na Mwanamke, amezaliwa chini ya sheria, kusudi awakomboe hao waliokuwa chini ya sheria, ili sisi tupokee hali ya kuwa wana wa Mungu(Gal 4:4,5)
Hata hivyo yesu hakija kuitangua torati (Mt.5:17)
JUMAPILI:-SIKU YA IBADA KATIKA AGANO JIPYA
Nilini wakristo walipoanza kuabudu siku ya kwanza ya juma, yaani Jumapili badala ya jumamosi?
Unabii ktk zaburi 118:22-24 unafafanuliwa ktk mahubiri ya Petro ktk matendo ya mitume 4:10-11 kuhusu Yesu.
Kwa kufufuka kwake amekuwa jiwe kuu la pembeni ,siku ya kufufuka kwake ndio iliotajwa kuwa ni "siku aliyoifanya Bwana, tutaishangilia na kuifurahia ",
Siku ya Sabato yaani (jumamosi) baada ya Yesu kufa kwake , Yesu Kristo alikuwa kaburini. Siku ya kwanza ya juma (jumapili) Yesu alifufuka kutoka kwa wafu! Haleluyaaa !!!!!! . kila alipojidhihirisha kwa wanafunzi wake ilikuwa ni ktk siku hiyo (mt 28:1-9, Yn 20:19, Lk 24:13-45, Yh 20:14-17 , kuwatokea hivyo mara kwa mara ktk siku za jumapili , haikuwa inatokea kwa bahati. Ilikusudiwa kuwafundisha kwamba siku hiyo, ya kufufuka Bwana ,kwa wakristo ni muhimu mno kwetu.
Katika siku hiyo ya kwanza ya juma , Yesu aliwavuvia wanafunzi wake wapokee Roho mtakatifu(Yh 20:19-22) Na ktika siku hiyo , siku yapentekoste Roho mtakatifu akawajia kwa mara ya kwanza ili kukaa ndani yao hata milele (mdo2:1-4) asomaye na afahamu . By W. S
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni