Naomba kujazia ktk mengi mazuri yaliyozungumzwa
=>jinsi gani au njia gani kwa vijana Wa Kike/ au Wa kiume kumpata mwenza Wa maisha?
Nimerudia swali makusudi ili niweze kueleweka zaidi.
1. WAKATI WA BWANA.
2. USIMPATE MWENZA NJE YA UWEPO WA MUNGU ILA KTK UWEPO WA MUNGU
3. NDOA NI MPANGO WA MUNGU NA MUNGU NDIYE MHUSIKA MKUU KATIKA KUTUUNGANISHA
1. *WAKATI WA BWANA* Mwanzo 2:18
Bwana akaona si vyema HUYU mtu awe peke yake akamfamyia msaidizi.
KUMBUKA kabla ya Mungu kusema Maneno haya, tayari Adamu aliumbwa Na alikuwa tayari amekwisha anza kuitenda kazi aliyopewa Na Mungu. (Hapa pia tunaona mke haikuwa sababu ya Adamu kuumbwa Adamu aliumbwa ili aitende kazi ya Mungu. Hivyo mwenza alikuja kama msaidizi katika kutimiza malengo Na makusudi Ya Mungu yeye kuumbwa hapa ulimwenguni.)
π embu kidogo turudi kwenye point hiihii ya kwanza. WAKATIπ€
Wakati ukifika Wa wewe kuolewa au kuoa hakika utaoa.
Tambua _"Mambo yote yamefungwa katika wakati''_
Mfalme sulemani anasema. _"Enyi Binti za Yerusalemu msiyachochee mapenzi hata yatakapokuja yenyewe''_π♂
=>Kutokea kuumbwa kwa Adamu hadi Eva kuumbwa kuna wakati mrefu kidogo. Ambao wakati wote huo Adamu alikuwa _"Anailima Na Kuitunza Bustani''_ mwanzo 2:15
Hivyo kitu chakwanza
*jiulize je huu ndiyo wakati sahihi Wa Mimi kuoa/kuolewa?*
2.Usimpate Mwenza nje ya UWEPO Wa Mungu.
Mazingira mliyokutana yanachangia kuwa Na ndoa iliyojaa majuto. Kama mmekutana kwenye uzinzi,ulevi, nk. Haya ni maxingira magumu mno ktk ndoa nyingi. Na ndoa hizi huishia kuvunjika au magomvi yasiyoisha.
Mfano Wa mazingira mazuri ya kukutana Na mwenza wako tunayaona kwa baba yetu Adamu. Mbele ya Mungu anakutana Na Mwenzi wake. Mungu anamletea (Mke mwema Toka kwa Bwana). Adamu anaamka usingizini Na kusema HUYU ni nyama katika nyama zangu mfupa ktk mifupa yangu (Mwanamke).
Aminaaa.
Hakika inapendeza wewe uliyedumu ktk kujitunza na unayehitaji kumpata mwenza wako Wa Maisha ukampata huyo mwenza kanisani. Au popote mkijishughulisha Na hbr au kazi iliyo halali mbele za Mungu.
Nimesema kazi iliyo halali kwa makusudi kabisa wala sijakosea
Maana kukutana Na mwenza wako ktk UWEPO WA MUNGU sio tu Kanisani au Kwe kwaya nk. Ila hata pengine mkiwa mnafanya shughuli za kila siku ambazo zampendeza Mungu.
MF.Rebecca alimpata mwenza kisimani alipoenda kuchota maji.π€
Sio eti mpo kilabuni mnakunywa pombe, au kwenye madangulo π€❗✖
3. Ndoa ni mpango Wa Mungu naye ndiye anayehusika kutuunganisha.
Ktk maeneo ambayo Mungu anahusika mwenyewe mojawapo ni hili.
Sio kwaakili zetu tunaweza kumpata mke/ Mme mwema Na anayestahili kuwa mwenzi wako Wa maisha.
Mungu NDIYE aliye husika kuona uhitaji Wa Adamu.
Hata kabla Adamu hajaona kwamba anauhitaji Mungu alimwona. Na Mara moja akaingia kazini kumfanyia msaidizi Wa kufanana naye....soma *Mwanzo 2:18*
Uhitaji Wa kupata msaidizi Bosi NDIYE ajuaye. Kwamba kazi Na jukumu alilokupa unahitaji msaidizi au LA!!!
Ndiyo
Narudia tena *Uhitaji Wa kupata msaidizi Bosi NDIYE ajuaye. Kwamba kazi Na jukumu alilokupa unahitaji msaidizi au LA!!!*
Tutambue hakika ya kwamba tumekuja Duniani tukiwa tumebeba kusudi la Mungu ndani yetu.
Na ikimpendeza Mungu hatuondoki hadi tulitimize.
Sasa hilo kusudi ndilo litaamua wewe uwe Na msaidizi au usiwe nae.
Na kama ni kuwa Na msaidizi awe Wa namna gani.
Mungu akasema natumfanyie msaidizi Wa *kufanana naye*
Maana yake atakayeeweza kuendana nawe Na kukusaidia kulibeba hilo kusudi la Mungu lililopo ndani yako.
Na hapa tunaona wengine wanaishia maisha yao yote bila kuwa Na mwenza hata aombeje hawezi pata.
Mfano Mkubwa ni kwa Yesu Kristo Na Yohana Mbatizaji.
Hawa wote wawili walibeba kusudi maalumu Na kwa wakati Maalumu. Na ilipofika muda Wa kazi umekamilika waliondoka zao.
Bado naona hujanielewa vizuri.
Embu hujawahi kutana Na mstari huu usemao
_"" Mbinguni hakuna kuoa wala kuolewa''_
Pia _"Sisi sote tuu bibi arusi Wa Bwana Yesu Kristo''_
Hapo sasa unaanza kuelewa.
Ni hivi kuoa au kuolewa ni neema Na mpango kamili Wa Mungu.
Kama umepangiwa kuoa au kuolewa haina haja ya kukimbilia au kukata tamaa utafika wakati alioupanga Bwana nawe utakuwa Na mwenza.
Pia kwa wewe ambae huna mwenza sio kwamba Mungu amekuacha au wewe ni mwenye dhambi sana kuliko mwengine la. Wewe ni Wa dhamani sana mbele za Mungu.
Na kwa wewe unayetafuta tambua kwamba unapaswa kutenga muda mwingi kuutafuta USO Wa Mungu Na kumwomba juu ya suala hilo.
Mungu awabariki mno.
Imeandaliwa Na Mtumishi Johnson Pokeaeli
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni