Jumanne, 6 Novemba 2018

SABABU ZINAZOFANYA KUTOJIBIWA MAOMBI YAKO

 SABABU ZINAZOFANYA KUTOJIBIWA MAOMBI YAKO

Tuliangalia sababu tano kwa kuzipitia tu zilikuwa hizi,

1. *KUTOMSAMEHE MTU MOYONI MWAKO*
Marko 11:25,26

2. *KUTOKUWA NA UHAKIKA WA IMANI YAKO KWA MUNGU JUU YA UNACHOKIOMBA*
Yakobo 1:5-7

3. *KUKATA TAMAA NA KUKOSA MSUKUMO WA KUOMBA NDANI YAKO*
Luka 18:1,7,8

4. *MATUMIZI MABAYA YA VITU UPEWAVYO NA MUNGU*
Yakobo 4:3

5. *JIBU LA MAOMBI YAKO KUFUNGIWA NDANI YA WAKATI ULIOAMRIWA*
Danieli 9:24

Unaeza kupitia na maandiko hayo kwa maelezo zaidi.
Leo tunasonga mbele na sababu zingine tano zaidi zinazofanya usijibiwe maombi yako.

Semina hii ni kwaajii yako
Twende pamoja.
[11/3, 19:11] Humphrey Mrema Arusha JHC ADMIN: SABABU YA SITA
6⃣ *HALI YAKO YA KIROHO KUWA CHINI AU NDOGO KULINGANA NA HITAJI LAKO KWA MUNGU.*

Wagalatia 4:1
. Lakini nasema ya kuwa mrithi, wakati wote awapo mtoto, hana tofauti na mtumwa, angawa ni bwana wa yote;

Wagalatia 4:2
. bali yu chini ya mawakili na watunzaji, hata wakati uliokwisha kuamriwa na baba.


Je! Huwa unakimbilia nyama wakati maziwa hujanywa? (Ebrania 5:13)
Kiwango chako cha Kiroho kinaendana na unachokiomba kwa Mungu? Jitathmini.
[11/3, 19:15] Humphrey Mrema Arusha JHC ADMIN:
SABABU YA SABA
7⃣ *KUHITAJIKA KWA MAOMBI YA KUFUNGA KUOMBEA JAMBO HILO LAKINI HUKUFUNGA*

Matayo 17:21
. [Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.]

Kwa wakati mwingine maombi ya kufunga ni kama KUKATA RUFAA. Hivyo ili upokee baadhi ya majibu ya maombi yako lazima ufunge kwa maombi.
Tafakari hilo!
[11/3, 19:22] Humphrey Mrema Arusha JHC ADMIN: SABABU YA NANE.
8⃣ *KIWANGO CHA NGUVU ZA MUNGU ZINAZOTENDA KAZI NDANI YAKO KUWA NDOGO KULINGANISHA NA JAMBO UNALOLIOMBEA.

Waefeso 3:20
. Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu;

Nifanyaje?? Omba Mungu akujaze nguvu zake za kutosha  ili azitumie kujibu maombi yako
Kwasababu *"...... kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana akiomba kwa bidii."* Yakobo 5:16
Maombi yako yanaachilia Nguvu inayotenda kazi kufungua vifungo na kujibu maombi.
[11/3, 19:30] Humphrey Mrema Arusha JHC ADMIN:
SABABU YA TISA
9⃣ *KUTOPANGILIA VIZURI MFUMO WA VIPAUMBELE VYAKO KI-MAISHA KAMA.  MUNGU ANAVYOTAKA NA UTEKELEZAJI MBOVU WA VIPAUMBELE VYA MUNGU MAISHANI MWAKO.*

Matayo 6:33
. Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.

Matayo 6:31
. Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini?

Je! Una vipaumbele gani vya kimaisha? Ukimweka Mungu kuwa kipaumbele nae ataweka mahitaji yako kuwa kipaumbele.
Wakati mwingine anachelewa kujibu maombi yako kwasababu hujampa kipaumbele ndio sababu.
Tutafakari vyema
[11/3, 19:40] Humphrey Mrema Arusha JHC ADMIN: SABABU YA KUMI
1⃣0⃣ *KUTOMZALIA MUNGU MATUNDA ANAYOTAKA YA KUDUMU.*

Yohana 15:16
. Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lo lote mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni

Matunda haya ni kama
--> _Tunda la Haki_ (Yakobo 3:18)

--> _Tunda la midomo_ (Ebr 13:15)

--> _Tunda la Roho_ (Galatia 5:22,23)

--> _Tunda la kazi_ (Wafilipi 1:22)

--> _Tunda la Toba_ (Mathayo 3:8)

Mzalie Mungu Matunda aone faida yako na kushawishika kukutendea makuu.


πŸ€πŸ€πŸ€
Follow us
*Instagram* joyfulhouseinchrist
*Facebook* Joyful House In Jesus Christ
*Blog* christiansforum1.blogspot.com
πŸ“§Or send us Email on
joyfulhouseinchrist@gmail.com

πŸ’’πŸ™πŸΌπŸŒΏ
©Nov.2018 Joyful House In Christ

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni