Leo nimetoka na hiki ibadani.
✍🏼TUNZA HUDUMA YAKO NA KUWA MWAMINIFU
Luka 25:13-30
13 Basi kesheni, kwa sababu hamwijui siku wala saa..........
Huu ni mfano juu ya talanta(talents) zilizogawanywa kwa watumwa ambao ndio sisi.
Ni kweli kama tulivyo viungo kila mmoja kwa mwenziwe tunatakiwa tuuhifadhi utumishi wetu kwa jambo lolote usiharibiwe bali huduma na karama na vipawa vikazae mara dufu.
Ukisoma vizuri pale anasema mwenye tano alileta kumi na mwenye mbili alileta nne Bwana wao akafurahi na kuwaambia waingie rahani.
Je uko tayari kuingia rahani kwa kuwa mwaminifu ???
Yule aliyepewa moja akaifukia kilichomkuta akanyanganywa hata kile kidogo na akatupwa nje mateso makali kilio na kisaga meno ikawa mshahara wake kwa sababu hakuwa mwaminifu na aliona kama hakuna faida bora kuifukia huduma yake.
Chagua sasa kuwa mwaminifu hata kufa ili taji yako ukaipate isiwe ndoto na talanta hizo zina hesabu yake mwisho kuwa mwaminifu isionekane hasaraa bali faida.
Kuna watu wanahitaji hata kuona tu unashauri vizuri nao wakavutwa kwa Yesu mshauri wa ajabu.
Ameen.
Tarehe 11/11/2018 kutoka kanisani Na Mtumishi Dalton
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni