ππ *GOOD MORNING JHC*πππΌ
_Tar. 7/1/2019 Neno fupi la Asubuhi_
Kichwa: *GHARAMA YA UOVU*
_Heri ya Mwaka Mpya wana Joyful House In Christ._
Mwanzo 3: _14 _"BWANA Mungu akamwambia nyoka, Kwa sababu umeyafanya hayo, umelaaniwa wewe kuliko wanyama wote, na kuliko hayawani wote walioko mwituni; kwa tumbo utakwenda, na mavumbi utakula siku zote za maisha yako; 15 nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino 16 Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto; na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala. 17 Akamwambia Adamu, Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nalikuagiza, nikisema, Usiyale; ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako; 18 michongoma na miiba itakuzalia, nawe utakula mboga za kondeni 19 kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi.''_
Gharama: Neno hili linasimama ikionyesho uzito Wa kitu Fulani . kwasababu unahitaji/kwasababu umefanya kitu Fulani hivyo unapaswa kulipa au kutembea katika hali Fulani.
✍✍
Twende sawa hapa:
Katika somo tulilosoma tunaona dhambi kubwa Na ya kwanza Mwanadamu aliyoitenda pale bustanini Na hii ikasababisha mpango mzima alioupanga Mungu Wa Mwanadamu kuishi maisha ya furaha Na ushindi. Kula bila kukitolea jasho chakula kile, kuzaa pasipo Na uchungu mkali, kuishi Kwa upendo Na amani pamoja Na viumbe wengine pasipo kuviogopa wala kudhurika.
Haya yote yalibadilika pale tu dhambi ilipotendeka. Adamu alipokula tunda la mti aliokatazwa asile.
Tunaona Mwanadamu baada ya dhambi ile hukumu ikatolewa Nayo ni ya kulipa gharama ya dhambi. Kwasababu alitenda dhambi kifo kikaingia, kuzaa Kwa uchungu, uadui kati ya mnyama Na mwanadamu ukawepo. Yote hii ni gharama ya Dhambi.
Katika maisha yetu, kuna hali au maisha ya baraka Na ushindi ambayo tulipaswa kuyaishi. Tulipaswa kuyafikia lakini kwasababu ya dhambi tunazo tenda zimekuwa kikwazo Na zikatuletea laana badala ya Baraka.
*Mshaara Wa Dhambi ni mauti*
Biashara yako ilipaswa kuwa ya viwango vya juu lakini upo hapohapo tu uendelei Na inawezekana ukiiangalia inashuka badala ya kuendelea tafakari ni wapi ulianguka, ni wapi ulimkosea Mungu ukatubu.
*Dhambi zetu zinatutenga mbali Na USO Wa Mungu*
Mpendwa kama unahitaji USO Wa Mungu uwe nawe katika maisha yako yote Naye akupe raha, akupe furaha,. Kama unahitaji mwaka huu 2019 uwe mwaka Wa kuinuliwa kwako Na kutoka katika hali ngumu uliyokuwa Nayo Kwa muda mrefu lamda ni ugonjwa au ulihitaji mtoto nk. Kama unahitaji ulinzi Wa Mungu katika kazi, biashara Na familia yako kubali leo kuacha yote ya Shetani Na Kumfuata Mungu. Mkiri Kristo kuwa Bwana Na Mwokozi Wa Maisha yako. Acha Dhambi Nate Bwana hato kuacha.
Barikiwa mpendwa
✍ Mwandaaji Wa somo Leo _Mtumishi Johnson Pokeaeli_
ππΌπ
©Jan 2019 Joyful House in Christ
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni