[1/7, 15:43] JHC: *SURA YA 11*
1 Nchi yote ilikuwa na lugha moja na usemi mmoja.
2 Ikawa watu waliposafiri pande za mashariki waliona nchi tambarare katika nchi ya Shinari; wakakaa huko.
3 Wakaambiana, Haya, na tufanye matofali tukayachome moto. Walikuwa na matofali badala ya mawe, na lami badala ya chokaa.
4 Wakasema, Haya, na tujijengee mji, na mnara, na kilele chake kifike mbinguni, tujifanyie jina; ili tusipate kutawanyika usoni pa nchi yote.
6 BWANA akasema, Tazama, watu hawa ni taifa moja, na lugha yao ni moja; na haya ndiyo wanayoanza kuyafanya, wala sasa hawatazuiliwa neno wanalokusudia kulifanya.
7 Haya, na tushuke huko, tuwachafulie usemi wao ili wasisikilizane maneno wao kwa wao.
8 Basi BWANA akawatawanya kutoka huko waende usoni pa nchi yote; wakaacha kuujenga ule mji.
9 Kwa sababu hiyo jina lake likaitwa Babeli; maana hapo ndipo BWANA alipoichafua lugha ya dunia yote; na kutoka huko BWANA akawatawanya waende usoni pa nchi yote.
10 Hivi ndivyo vizazi vya Shemu; Shemu alikuwa mtu wa miaka mia akamzaa Arfaksadi miaka miwili baada ya gharika.
11 Shemu akaishi baada ya kumzaa Arfaksadi miaka mia tano, akazaa wana, waume na wake.
12 Arfaksadi akaishi miaka thelathini na mitano, akamzaa Sela.
13 Arfaksadi akaishi baada ya kumzaa Sela miaka mia nne na mitatu, akazaa wana, waume na wake.
14 Sela akaishi miaka thelathini, akamzaa Eberi.
15 Sela akaishi baada ya kumzaa Eberi miaka mia nne na mitatu, akazaa wana, waume na wake.
16 Eberi akaishi miaka thelathini na minne, akamzaa Pelegi.
17 Eberi akaishi baada ya kumzaa Pelegi miaka mia nne na thelathini, akazaa wana, waume na wake.
18 Pelegi akaishi miaka thelathini, akamzaa Reu.
19 Pelegi akaishi baada ya kumzaa Reu miaka mia mbili na kenda, akazaa wana, waume na wake.
20 Reu akaishi miaka thelathini na miwili, akamzaa Serugi.
21 Reu akaishi baada ya kumzaa Serugi miaka mia mbili na saba, akazaa wana, waume na wake.
22 Serugi akaishi miaka thelathini, akamzaa Nahori.
23 Serugi akaishi baada ya kumzaa Nahori miaka mia mbili, akazaa wana, waume na wake.
24 Nahori akaishi miaka ishirini na kenda, akamzaa Tera.
25 Nahori akaishi baada ya kumzaa Tera miaka mia na kumi na kenda, akazaa wana, waume na wake.
26 Tera akaishi miaka sabini, akamzaa Abramu, na Nahori, na Harani.
27 Na hivi ndivyo vizazi vya Tera. Tera akamzaa Abramu, na Nahori, na Harani. Harani akamzaa Lutu.
28 Harani akafa kabla ya baba yake Tera katika nchi aliyozaliwa, yaani, katika Uru wa Wakaldayo.
29 Abramu na Nahori wakajitwalia wake. Jina la mkewe Abramu aliitwa Sarai, na jina la mkewe Nahori aliitwa Milka, binti Harani, ambaye alikuwa baba wa Milka na wa Iska.
30 Na Sarai alikuwa tasa, hakuwa na mtoto.
31 Tera akamtwaa Abramu mwanawe, na Lutu mwana wa Harani, mwana wa mwanawe, na Sarai mkwewe, mke wa Abramu mwanawe, wakatoka wote katika Uru wa Wakaldayo, waende nchi ya Kanaani, wakafika mpaka Harani wakakaa huko.
32 Siku za Tera zilikuwa miaka mia mbili na mitano; Tera akafa katika Harani.
[1/7, 20:46] JHC: *KITABU CHA MWANZO SURA YA 12*
1 BWANA akamwambia Abramu, Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha;
2 nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka;
3 nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa.
5 Abramu akamchukua Sarai mkewe, na Lutu mwana wa nduguye, na vitu vyao vyote walivyokuwa wamejipatia na hao watu waliowapata huko Harani, wakatoka ili kwenda nchi ya Kanaani; nao wakaingia katika nchi ya Kanaani.
6 Abramu akapita katikati ya nchi mpaka mahali patakatifu pa Shekemu; mpaka mwaloni wa More. Na Wakanaani siku zile walikaa katika nchi hiyo.
7 BWANA akamtokea Abramu, akasema, Uzao wako nitawapa nchi hii. Naye huko akamjengea madhabahu BWANA aliyemtokea.
8 Kisha akaondoka huko akaenda mpaka mlima ulio upande wa mashariki wa Betheli, akaipiga hema yake; alikuwa na Betheli upande wa magharibi, na Ai upande wa mashariki, akamjengea BWANA madhabahu huko, akaliitia jina la BWANA.
9 Naye Abramu akasafiri, akazidi kwenda pande za kusini.
10 Basi kulikuwa njaa katika nchi ile; Abramu akashuka Misri, akae huko kwa muda maana njaa ilikuwa nzito katika nchi.
11 Ikawa alipokuwa karibu kuingia Misri, akamwambia Sarai mkewe, Tazama, najua ya kuwa u mwanamke mzuri wa uso;
12 basi itakuwa, Wamisri watakapokuona watasema, Huyu ni mkewe; kisha wataniua mimi na wewe watakuacha hai.
13 Tafadhali useme, wewe u ndugu yangu, iwe heri kwangu kwa ajili yako, na nafsi yangu iishi kwa ajili yako.
14 Basi ikawa Abramu alipofika Misri, Wamisri wakamwona huyo mwanamke ya kwamba yeye ni mzuri sana.
15 Wakuu wa Farao wakamwona, nao wakamsifu kwa Farao; basi yule mwanamke akachukuliwa nyumbani mwa Farao.
16 Naye akamtendea Abramu mema kwa ajili yake; naye alikuwa na kondoo na ng’ombe, na punda waume, na watumwa, na wajakazi, na punda wake, na ngamia.
17 Lakini BWANA akampiga Farao na nyumba yake mapigo makuu, kwa ajili ya Sarai, mkewe Abramu.
18 Ndipo Farao akamwita Abramu, akasema, N’nini hili ulilonitendea? Mbona hukuniambia ya kuwa huyo ni mkeo?
19 Mbona ulisema, Huyo ni umbu langu, hata nikamtwaa kuwa mke wangu? Basi sasa, huyo mke wako umchukue, uende zako.
20 Farao akawaagiza watu kwa ajili yake, wakampeleka njiani, na mkewe, na kila alichokuwa nacho.
[1/8, 15:46] JHC: Sura ya 11 inazungumza juu ua Habari za Mnara Wa Babeli Na sababu ya uwepo Wa Lugha nyingi duniani.
Pia inawaonyesha Abramu, Harani Na Nahori ambao ni ndugu watoto Wa Baba mmoja ambaye ni Tera.
Si hivyo tu inaonyesha pia juu ya habari ya Safari ya kutoka Nchi iitwayo HURU WA KALDAYO KWENDA KANAANI.
safari hii ilianza kabla ya wito
[1/8, 16:04] JHC: Habari za Abramu na Baraka zake pamoja Na uzao wake zinaanza katika sura hii ya 12.
""Mungu atambariki ambarikie Na amlaanie atamlaani.'''
Baraka hii ni ya ajabu sana pia ni Baraka ambayo ilimhakikishia Abramu ulinzi Na Usalama popote apitapo.
Kwa yeyote atakayemgusa amegusa mboni ya jicho LA Mungu.
Hivyo kama amemjerui Abramu au kumchukulia chochote chake basi Mungu hatomwacha huyo adui salama.
Na hayo tunayaona yakianza kutimia kwenye kisa kilichoandikwa hapo cha Farao kumchukua Mke Wa Abramu. Kitu kilichotokea ni adhabu Kwa Farao Na nyumba Yake yote hadi alipomwachia yule Mke Wa watu. Na kuwaruhusu waondoke Kwa amani
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni