Jumanne, 8 Januari 2019

KITABU CHA MWANZO 15-16

[1/8, 20:36] JHC: *KITABU CHA MWANZO SURA YA 15-16*   _Shalom Wapendwa karibuni tumalizie sehemu ya leo ambapo leo tutakuwa tumesoma Sura ya 13-16. Mungu akubariki_†



1 Baada ya mambo hayo neno la BWANA likamjia Abramu katika njozi, likinena, Usiogope, Abramu, Mimi ni ngao yako, na thawabu yako kubwa sana.
2 Abramu akasema, Ee Bwana MUNGU, utanipa nini, nami naenda zangu hali sina mtoto, na atakayeimiliki nyumba yangu ni huyu Eliezeri, Mdameski?
3 Abramu akasema, Tazama, hukunipa uzao, na mtu aliyezaliwa nyumbani mwangu ndiye mrithi wangu.
4 Nalo neno la BWANA likamjia likinena, Huyu hatakurithi, bali atakayetoka katika viuno vyako ndiye atakayekurithi.
5 Akamleta nje, akasema, Tazama sasa mbinguni, kazihesabu nyota, kama ukiweza kuzihesabu. Akamwambia, Ndivyo utakavyokuwa uzao wako.
6 Akamwamini BWANA, naye akamhesabia jambo hili kuwa haki.
7 Kisha akamwambia, Mimi ni BWANA, niliyekuleta kutoka Uru wa Wakaldayo nikupe nchi hii ili uirithi.
8 Akasema, Ee Bwana MUNGU, nipateje kujua ya kwamba nitairithi?
9 Akamwambia, Unipatie ndama wa miaka mitatu, na mbuzi mke wa miaka mitatu, na kondoo mume wa miaka mitatu, na hua, na mwana njiwa.
10 Akampatia hao wote, akawapasua vipande viwili, akaweka kila kipande kuelekea mwenzake, ila ndege hakuwapasua.
11 Hata tai walipotua juu ya mizoga Abramu akawafukuza.
12 Na jua lilipokuwa likichwa usingizi mzito ulimshika Abramu, hofu ya giza kuu ikamwangukia.
13 BWANA akamwambia Abramu, Ujue hakika ya kwamba uzao wako utakuwa mgeni katika nchi isiyo yake, watawatumikia watu wale, nao watateswa muda wa miaka mia nne.
14 Hata na taifa lile, watakaowatumikia, nitawahukumu; baadaye watatoka na mali mengi.
15 Lakini wewe utakwenda kwa baba zako kwa amani, utazikwa katika uzee mwema.
16 Na kizazi cha nne kitarudi hapa, maana haujatimia uovu wa Waamori bado.
17 Ikawa, jua lilipokuchwa likawa giza, tazama, tanuru ya moshi na mwenge unaowaka ulipita kati ya vile vipande vya nyama.
18 Siku ile BWANA akafanya agano na Abramu, akasema, Uzao wako nimewapa nchi hii, kutoka mto wa Misri mpaka huo mto mkubwa, mto Frati,
19 Mkeni, na Mkenizi, na Mkadmoni,
20 na Mhiti, na Mperizi, na Mrefai,
🌺
*SURA YA* 1⃣6⃣

1 Basi Sarai mkewe Abramu hakumzalia mwana, naye alikuwa na mjakazi, Mmisri, jina lake Hajiri.
2 Sarai akamwambia Abramu, Basi sasa, BWANA amenifunga tumbo nisizae, umwingilie mjakazi wangu labda nitapata uzao kwa yeye. Abramu akaisikiliza sauti ya Sarai.
3 Sarai mkewe Abramu akamtwaa Hajiri Mmisri mjakazi wake, baada ya kukaa Abramu katika nchi ya Kanaani miaka kumi, akampa Abramu mumewe, awe mkewe.
4 Basi akamwingilia Hajiri, naye akapata mimba. Naye alipoona ya kwamba amepata mimba, bibi yake alikuwa duni machoni pake.
5 Sarai akamwambia Abramu, Ubaya ulionipata na uwe juu yako; nimekupa mjakazi wangu kifuani mwako, naye alipoona kwamba amepata mimba, mimi nimekuwa duni machoni pake. BWANA na ahukumu kati ya mimi na wewe.
6 Naye Abramu akamwambia Sarai, Tazama, mjakazi wako yu mkononi mwako, mtendee lililo jema machoni pako. Sarai akamtesa, naye akakimbia kutoka mbele yake.
7 Malaika wa BWANA akamwona kwenye chemchemi ya maji katika jangwa, chemchemi iliyoko katika njia ya kuendea Shuri.
8 Akamwambia, Hajiri, wewe mjakazi wa Sarai, unatoka wapi, nawe unakwenda wapi? Akanena, Nakimbia mimi kutoka mbele ya bibi yangu Sarai.
9 Malaika wa BWANA akamwambia, Rudi kwa bibi yako, ukanyenyekee chini ya mikono yake.
10 Malaika wa BWANA akamwambia, Hakika nitauzidisha uzao wako, wala hautahesabika kwa jinsi utakavyokuwa mwingi.
11 Malaika wa BWANA akamwambia, Tazama! Wewe una mimba, utazaa mwana wa kiume, nawe utamwita jina lake Ishmaeli, maana BWANA amesikia kilio cha mateso yako.
12 Naye atakuwa kama punda-mwitu kati ya watu, mkono wake utakuwa juu ya watu wote na mkono wa watu wote utakuwa juu yake, naye atakaa mbele yao ndugu zake wote.
13 Akaliita jina la BWANA aliyesema naye, Wewe U Mungu uonaye, kwani alisema, Hata hapa nimemwona yeye anionaye?
14 Kwa hiyo kisima kile kiliitwa Beer-lahai-roi. Tazama, kiko kati ya Kadeshi na Beredi.
15 Hajiri akamzalia Abramu mwana wa kiume; Abramu akamwita jina lake Ishmaeli, yule mwanawe, ambaye Hajiri alimzaa.
16 Naye Abramu alikuwa mtu wa miaka themanini na sita, hapo Hajiri alipomzalia Abramu Ishmaeli.

© Jan  2019 *Joyful House in Christ*
[1/8, 21:04] JHC: Embu tutazame Sura hizi mbili tena sura ya 15-16
*"USIOGOPE ABRAMU MIMI NI NGAO YAKO NA THAWABU YAKO KUBWA SANA''* 15: 1

Haleluya.
Sura ya 15 inaanza Kwa maneno mazuri Na yenye kumfariji Abramu, Yanamtia nguvu, Na kumhakikishia kwamba Mungu yupo ktk safari yake.

Abramu alikuwa Na hofu akitazama Mali Na utajiri Mkubwa aliokuwa nao aliingiwa Na wasiwasi kwamba ni nani atakayeuridhi? Na alikuwa bado hajapata mtoto Na Umri ushaenda sana.
[1/8, 21:15] JHC: Katika Sura ya 16 tunaona namna uvumilivu unahitajika katika kungoja ahadi ya Mungu. Ahadi ya Mungu usiitazame Kwa macho ya Kibinadamu. Hitaji uongozi Wa Roho Mtakatifu. Abramu waliona miaka 86 ni mingi hivyo wakatafuta shortcut ili wapate mtoto Na iumbe wanamkosea Mungu.

-Lakini tunaona pia unyanyasaji Mkubwa Sarai anaufanya Kwa mama Yake Ishamael. Na hadi anachukua hatua ya kukimbia. Inatupasa tufikiri kabla ya kutenda. Sarai ndiye aliyehitaji Mumewe awe Na mtoto Na akampatia Hajiri ili amwoe Na amzalie mtoto. Lakini baada ya Hajiri kupata mimba. Sarai anaona wivu Na iumnyanyasa. Loo Mungu aturehemu.

Wapendwa yapo mengi tunayapata katika kila eneo tunalosoma. Ila Mungu atubariki Kwa haya machache tuliyoyapata.


Nakukaribisha kesho tuendelee Na Sura ya 17-20.
πŸ™πŸΌπŸ’’πŸ’’πŸ’’πŸ’’
Aidha speed yetu ni nzuri sana Chamuhimu usiache Kiporo jitahidi ratiba ya Leo uimalize ili kesho usiwe Na mzigo Mkubwa.

BarikiwaπŸ’’πŸ’’πŸ’’πŸ’’πŸ’’

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni