[1/7, 10:16] JHC: *KITABU CHA MWANZO SURA YA 9*
💒🍀
1 Mungu akambariki Nuhu na wanawe, akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi.
2 Kila mnyama wa katika nchi atawaogopa ninyi na kuwahofu, na kila ndege wa angani: pamoja na vitu vyote vilivyojaa katika ardhi, na samaki wote wa baharini; vimetiwa mikononi mwenu.
3 Kila kiendacho kilicho hai kitakuwa chakula chenu, kama nilivyowapa mboga za majani, kadhalika nawapeni hivi vyote.
4 Bali nyama pamoja na uhai, yaani, damu yake, msile.
5 Hakika damu yenu ya uhai wenu nitaitaka; na kwa mkono wa kila mnyama nitaitaka; na kwa mkono wa mwanadamu, kwa mkono wa ndugu ya mtu nitataka uhai wa mwanadamu.
6 Atakayemwaga damu ya mwanadamu, damu yake huyo itamwagwa na mwanadamu, maana kwa mfano wake Mungu alimfanya mwanadamu.
7 Nanyi zaeni, mkaongezeke; zaeni sana katika nchi, mkaongezeke ndani yake.
8 Mungu akamwambia Nuhu, na wanawe pamoja naye, akisema,
9 Mimi, tazama, nalithibitisha agano langu nanyi; tena na uzao wenu baada yenu;
10 tena na kila kiumbe hai kilichoko pamoja nanyi, ndege, na mnyama wa kufugwa, na kila mnyama wa mwitu katika nchi pamoja nanyi; wote wanaotoka katika safina, hata kila kilicho hai katika nchi.
11 Na agano langu nitalithibitisha nanyi; wala kila chenye mwili hakitafutwa tena kwa maji ya gharika; wala hakutakuwa tena gharika, baada ya hayo, kuiharibu nchi.
12 Mungu akasema, Hii ndiyo ishara ya agano nifanyalo kati yangu na ninyi, na kila kiumbe hai kilichoko pamoja nanyi, kwa vizazi vyote hata milele;
13 Mimi nauweka upinde wangu winguni, nao utakuwa ni ishara ya agano kati yangu na nchi.
14 Hata itakuwa nikitanda mawingu juu ya nchi, upinde utaonekana winguni,
15 nami nitalikumbuka agano langu, lililoko kati yangu na ninyi, na kila kiumbe hai katika wote wenye mwili, wala maji hayatakuwa gharika tena kuwaharibu wote wenye mwili.
16 Basi huo upinde utakuwa winguni; nami nitauangalia nipate kulikumbuka agano la milele lililoko kati ya Mungu na kila kiumbe hai katika wote wenye mwili kilichoko katika nchi.
17 Mungu akamwambia Nuhu, Hii ndiyo ishara ya agano nililoliweka kati yangu na wote wenye mwili walioko katika nchi.
18 Wana wa Nuhu waliotoka katika safina, ni Shemu, na Hamu, na Yafethi; na Hamu ndiye baba wa Kanaani.
19 Hawa watatu walikuwa wana wa Nuhu na kwa hao nchi yote ikaenea watu.
20 Nuhu akaanza kuwa mkulima, akapanda mizabibu;
21 akanywa divai, akalewa; akawa uchi katika hema yake.
22 Hamu, baba wa Kanaani, akauona uchi wa baba yake, akawaeleza ndugu zake wawili waliokuwa nje.
23 Shemu na Yafethi wakatwaa vazi, wakalitanda mabegani mwao wote wawili, wakaenda kinyumenyume, wakaufunika uchi wa baba yao; na nyuso zao zilielekea nyuma, wala hawakuuona uchi wa baba yao.
24 Nuhu akalevuka katika ulevi wake, akajua mwana wake mdogo alivyomtendea.
25 Akasema, Na alaaniwe Kanaani; Atakuwa mtumwa kabisa kwa ndugu zake.
26 Akasema, Na atukuzwe BWANA Mungu wa Shemu; Na Kanaani awe mtumwa wake.
27 Mungu akamnafisishe Yafethi. Na akae katika hema za Shemu; Na Kanaani awe mtumwa wake.
28 Na Nuhu akaishi baada ya ile gharika miaka mia tatu na hamsini.
29 Siku zote za Nuhu zilikuwa miaka mia kenda na hamsini, akafa.
©2019 JHC Reading Bible Campaign
[1/7, 14:27] JHC: *KITABU CHA MWANZO SURA YA 10*
1 Hivi ndivyo vizazi vya wana wa Nuhu, Shemu, na Hamu, na Yafethi. Na kwao walizaliwa wana wa kiume baada ya gharika.
2 Wana wa Yafethi ni Gomeri, na Magogu, na Madai, na Yavani, na Tubali, na Mesheki, na Tirasi.
3 Na wana wa Gomeri ni Ashkenazi, na Rifathi, na Togama.
4 Na wana wa Yavani ni Elisha, Tarshishi, Kitimu, na Warodani.
5 Kwa hao nchi za pwani za mataifa ziligawanyikana kuwa nchi zao, kila moja kwa lugha yake, kwa jamaa zao, kufuata mataifa yao.
6 Na wana wa Hamu ni Kushi, na Misri, na Putu, na Kanaani.
7 Na wana wa Kushi ni Seba, na Havila, na Sabta, na Raama, na Sabteka. Na wana wa Raama ni Sheba, na Dedani.
8 Kushi akamzaa Nimrodi, akaanza kuwa mtu hodari katika nchi.
9 Alikuwa hodari kuwinda wanyama mbele za BWANA. Kwa hiyo watu hunena, Kama Nimrodi, hodari wa kuwinda wanyama mbele za BWANA.
10 Mwanzo wa ufalme wake ulikuwa Babeli na Ereku, na Akadi, na Kalne, katika nchi ya Shinari.
11 Akatoka katika nchi ile akaenda mpaka Ashuru, akajenga Ninawi, na Rehoboth-iri, na Kala;
12 na Reseni, kati ya Ninawi na Kala, nao ni mji mkubwa.
13 Misri akazaa Waludi, na Waanami, na Walehabi, na Wanaftuhi,
14 na Wapathrusi, na Wakasluhi; huko ndiko walikotoka Wafilisti na Wakaftori.
15 Kanaani akamzaa Sidoni, mwanawe wa kwanza, na Hethi,
16 na Myebusi, na Mwamori, na Mgirgashi,
17 na Mhivi, na Mwarki, na Msini,
18 na Mwarvadi, na Msemari, na Mhamathi. Baadaye jamaa za Wakanaani walitawanyikana.
19 Na mpaka wa Wakanaani ulianza kutoka Sidoni kwa njia ya Gerari hata Gaza; tena kwa njia ya Sodoma, na Gomora, na Adma, na Seboimu, hata Lasha.
20 Hao ndio wana wa Hamu, kufuata jamaa zao, kwa lugha zao, katika nchi zao, kufuata mataifa yao.
21 Naye Shemu ambaye ni baba wa wana wote wa Eberi, na ndugu mkubwa wa Yafethi, akazaliwa wana.
22 Wana wa Shemu ni Elamu, na Ashuru, na Arfaksadi, na Ludi, na Aramu.
23 Na wana wa Aramu ni Usi, na Huli, na Getheri, na Mashi.
24 Arfaksadi akamzaa Sela, Sela akamzaa Eberi.
25 Eberi akazaliwa wana wawili wa kiume; jina la wa kwanza ni Pelegi maana katika siku zake nchi iligawanyika; na jina la nduguye ni Yoktani.
26 Yoktani akamzaa Almodadi, na Shelefu, na Hasarmawethi, na Yera,
27 na Hadoramu, na Uzali, na Dikla,
28 na Obali, na Abimaeli, na Seba,
29 na Ofiri, na Havila, na Yobabi. Hao wote ndio wana wa Yoktani.
30 Makao yao yalikuwa kutoka Mesha kwa njia ya Sefari, mlima wa mashariki.
31 Hao ndio wana wa Shemu, kufuata jamaa zao, na lugha zao, katika nchi zao, kufuata mataifa yao.
32 Hizo ndizo jamaa za wana wa Nuhu, kufuata vizazi vyao, katika mataifa yao; na kwa hao mataifa yaligawanyika katika nchi baada ya gharika.
[1/8, 15:15] JHC: Hapa tunaona kizazi kipya kutoka katika mbegu ambayo Mungu aliokoa. Aliihifadhi kwenye Safina
[1/8, 15:22] JHC: Kizazi/mbegu hiki kinapewa maagizo. Kikazaliane Na kuijaza nchi. Lakini kuna mambo wanayopaswa kuyafanya Na mengine hawapaswi kuyafanya.
Ukweli ni kwamba kutokea wakati Wa Kuumbwa Kwa ulimwengu Mungu anaonekana kuruhusu mambo mabaya yaendelee kuwepo. Anayaacha tu. Kama alivyoacha ule mti Wa ujuzi Wa mema Na mabaya pale bustanini. Hii yote ni kama kipimo Na mtihani Kwa Mwanadamu kumpima ni Kwa namna gani mwanadamu atakuwa mtii Na kumhofu Mungu. Ni Kwa namna gani Mwanadamu atamweshimu Mungu hata kama kuna vitu vinavutia Kwa namna gani lakini Mungu anataka Mwanadamu awe tayari kuviacha ili amfuate Yeye peke Yake. Yaani Mungu anataka ifikie mahali Mwanadamu aseme Pombe, Zinaa, kuiba, rushwa, kisusio, mchepuko, ni vizuri Na vinatamanisha lakini Mungu ni mzuri zaidi, kumcha Mungu kunatamanisha zaidi. Tukifikia hapo Hakika Mungu hufurahi
[1/8, 15:35] JHC: Katika Sura hii ya 10 tunaona mambo makubwa ambayo yanabeba historia ya Nchi Na Mataifa Na maeneo mbalimbali makubwa tunayoyaona yakirudiwa kwenye biblia kama vile Misri, Kanaan Na Tarshishi, Na Sheba.
Katika mwisho Wa sura ya Tisa Na Ile ya Kumi ndipo utaona kwamba kwanini Mataifa haya yamekuwa Na tabia tofauti tofauti, mengine baadae yatakuwa Na njaa Na kukimbilia Kwa wengine kutafuta chakula shida ilianza pale wale watoto au mababa Watatu Shemu, Hamu Na Yafeth mmoja alipomkosea Baba Yake Na Wawili walipomsitiri Baba Yake. Baba yao Nuhu alitoa Mbaraka Na laana. Na hii ikabaki juu ya hata kipindi cha kuzaliwa Kristo. Kristo Na Taifa LA Israel Mungu alilichagua kutoka kwenye watoto wa SHEMU
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni