[1/8, 11:53] JHC: KITABU CHA MWANZO SURA YA 13 NA 14
1 Abramu akapanda kutoka Misri, yeye, na mkewe, na kila alichokuwa nacho, na Lutu pamoja naye, mpaka kusini.
2 Naye Abramu alikuwa ni tajiri sana kwa mifugo, kwa fedha, na kwa dhahabu.
3 Akaendelea kusafiri kutoka kusini mpaka Betheli, mahali pale palipokuwapo hema yake kwanza kati ya Betheli na Ai;
4 napo ndipo palipokuwa na madhabahu aliyofanya hapo kwanza; naye Abramu akaliitia jina la BWANA hapo.
5 Na Lutu aliyesafiri pamoja na Abramu, yeye naye alikuwa na makundi ya ng’ombe na kondoo, na hema.
6 Na ile nchi haikuwatosha, ili wakae pamoja; maana mali zao zilikuwa nyingi, hata wasiweze kukaa pamoja.
7 Kukawako ugomvi kati ya wachunga wanyama wa Abramu, na wachunga wanyama wa Lutu; na siku zile Wakanaani na Waperizi walikuwa wakikaa katika nchi.
8 Abramu akamwambia Lutu, Basi, usiwepo ugomvi, nakusihi, kati ya mimi na wewe, wala kati ya wachungaji wangu na wachungaji wako; maana sisi tu ndugu.
9 Je! Nchi hii yote haiko mbele yako? Basi ujitenge nami, nakusihi; ukienda upande wa kushoto, nitakwenda upande wa kuume; ukienda upande wa kuume, nitakwenda upande wa kushoto.
10 Lutu akainua macho yake, akaliona Bonde lote la Yordani, ya kwamba lote pia lina maji, kabla BWANA hajaharibu Sodoma na Gomora, lilikuwa kama bustani ya BWANA, kama nchi ya Misri hapo unapokwenda Soari.
11 Basi Lutu akajichagulia Bonde lote la Yordani; Lutu akasafiri kwenda upande wa mashariki; wakatengana wao kwa wao.
12 Abramu akakaa katika nchi ya Kanaani, na Lutu akakaa katika miji ya lile Bonde; akajongeza hema yake mpaka Sodoma.
13 Lakini watu wa Sodoma walikuwa wabaya, wenye kufanya dhambi nyingi sana juu ya BWANA.
14 BWANA akamwambia Abramu, alipokwisha kutengana na Lutu, Inua sasa macho yako, ukatazame kutoka hapo ulipo, upande wa kaskazini, na wa kusini na wa mashariki na wa magharibi;
15 maana nchi hii yote uionayo, nitakupa wewe na uzao wako hata milele.
16 Na uzao wako nitaufanya uwe kama mavumbi ya nchi; hata mtu akiweza kuyahesabu mavumbi ya nchi, uzao wako nao utahesabika.
17 Ondoka, ukatembee katika nchi hii katika mapana yake, na marefu yake, maana nitakupa wewe nchi hiyo.
18 Basi Abramu akajongeza hema yake, akaja akakaa kwenye mialoni ya Mamre, nayo ni miti iliyoko Hebroni, akamjengea BWANA madhabahu huko.
ππΌππΌππΌπΊπ♂
*SURA YA 14*
1 Ikawa siku za Amrafeli mfalme wa Shinari, na Arioko mfalme wa Elasari, na Kedorlaoma mfalme wa Elamu na Tidali mfalme wa Goimu,
2 walifanya vita na Bera mfalme wa Sodoma na Birsha mfalme wa Gomora, na Shinabu mfalme wa Adma, na Shemeberi mfalme wa Seboimu, na mfalme wa Bela, ndio Soari.
3 Hawa wote wakakutana panapo bonde la Sidimu, kwenye Bahari ya Chumvi.
4 Miaka kumi na miwili walimtumikia Kedorlaoma, hata mwaka wa kumi na tatu wakaasi.
5 Na mwaka wa kumi na nne akaja Kedorlaoma na wafalme waliokuwa pamoja naye, wakawapiga Warefai katika Ashteroth-karnaimu, na Wazuzi katika Hamu, na Waemi katika Shawe-kiryathaimu,
6 na Wahori katika mlima wao Seiri, mpaka Elparani iliyo karibu na jangwa.
7 Kisha wakarudi wakaja mpaka Enmisfati, ndio Kadeshi, wakapiga nchi yote ya Waamaleki, na Waamori waliokaa Hasason-tamari.
8 Mfalme wa Sodoma, na mfalme wa Gomora, na mfalme wa Adma, na mfalme wa Seboimu, na mfalme wa Bela, ndio Soari, wakatoka wakapanga vita panapo bonde la Sidimu;
9 wapigane na Kedorlaoma mfalme wa Elamu, na Tidali mfalme wa Goimu, na Amrafeli mfalme wa Shinari, na Arioko mfalme wa Elasari, wafalme wanne juu ya wale watano.
10 Na bonde la Sidimu lilikuwa limejaa mashimo ya lami. Nao wafalme wa Sodoma na Gomora wakakimbia, wakaanguka huko, nao waliosalia wakakimbia milimani.
11 Wakachukua mali zote za Sodoma na Gomora na vyakula vyao vyote, wakaenda zao.
12 Wakamtwaa Lutu, mwana wa nduguye Abramu, aliyekaa huko Sodoma, na mali yake, wakaenda zao.
13 Mtu mmoja aliyeponyoka akaenda, akampasha habari Abramu Mwebrania; naye amekaa panapo mialoni ya Mamre, yule Mwamori, ndugu ya Eshkoli, na ndugu ya Aneri, na hao walikuwa wamepatana na Abramu.
14 Abramu aliposikia ya kwamba nduguye ametekwa mateka, akawapa silaha vijana wake, waliozaliwa katika nyumba yake, watu mia tatu na kumi na wanane, akawafuata mpaka Dani.
15 Akajipanga apigane nao usiku, yeye na watumwa wake, akawapiga, akawafukuza mpaka Hoba, ulioko upande wa kushoto wa Dameski.
16 Naye akarudisha mali zote, akamrudisha na Lutu nduguye na mali zake, na wanawake pia, na watu.
17 Abramu aliporudi kutoka kumpiga Kedorlaoma na wale wafalme waliokuwa pamoja naye, mfalme wa Sodoma akatoka amlaki katika bonde la Shawe, nalo ni Bonde la Mfalme.
18 Na Melkizedeki mfalme wa Salemu akaleta mkate na divai, naye alikuwa kuhani wa Mungu Aliye juu sana.
19 Akambariki, akasema, Abramu na abarikiwe na Mungu Aliye juu sana, Muumba mbingu na nchi.
20 Ahimidiwe Mungu Aliye juu sana, aliyewatia adui zako mikononi mwako. Abramu akampa fungu la kumi la vitu vyote.
21 Mfalme wa Sodoma akamwambia Abramu, Nipe mimi hao watu, na hizo mali uchukue wewe.
22 Abramu akamwambia mfalme wa Sodoma, Nimeinua mkono wangu kwa BWANA, Mungu Aliye juu sana, Muumba mbingu na nchi,
23 ya kuwa sitatwaa uzi wala gidamu ya kiatu wala cho chote kilicho chako, usije ukasema, Nimemtajirisha Abramu;
24 isipokuwa hivyo walivyokula vijana, na sehemu za watu waliokwenda nami, yaani, Aneri, na Eshkoli, na Mamre; na watwae wao sehemu zao.
*Bwana akubariki Kwa kuungana nasi kusoma*
πππΌ
©2019 Joyful House in Christ
[1/8, 20:55] JHC: Bwana Yesu Asifiwe mpendwa wangu. Karibu tutafakari/ tucheuwe kidogo Yale tuliyosoma Siku ya Leo katika Sura hizi NNE za KITABU cha MWANZO.
Nianze Na Sura ya 13-14
-Tunaona Habari za Abramu akiwa ameshaingia kwenye Nchi ya Kanaani.
-Na anaiizunguka Nchi yote kusini, magharibi, mashariki Na Kaskazini.
Mungu anamwahidi kwamba Nchi hiyo atawapatia uzao Wa Abramu.
-Lakini ikumbukwe kwamba bado Tumbo la Sarai mkewe lilikuwa bado ni Tasa. Yaani hana mtoto bado.
- Mungu anamwonyesha Utajiri uliopo kwenye Nchi ile.
-Nchi iliyojaa Asali Na Maziwa.
Katika kuizunguka Nchi ile Na kuishi kwake Abramu pale akiwa pamoja Na Mjomba wake yaani Lutu mtoto Wa kaka Yake. Wote wanatajirika sana sana. Na baadae wakaona wasitembee pamoja watengane.
- Jambo jingine tunaloliona ni kwamba Mungu analeta Ushindi Na Wokovu kupitia Mkono Wa Abramu baada ya kwenda kumwokoa Ndugu Yake Kule alipokuwa ametekwa mateka.
-jambo kubwa tujifunze Kutoka Kwa Abramu ni Shukrani Na Kuthamini nguvu za Mungu juu ya kila tunalolifanya. Tusijichukulie utukufu. Abramu hakujichukulia utukufu hakujisifu kwamba yeye ndiye aliyewaokoa Lutu Na watu wengine Na Mali zao Bali ni Bwana.
Na anamtolea Bwana Sadaka ya Fungu LA Kumi.
Alitoa Kwa hiyari sio Kwa kulazimishwa kama wengi wanavyotaka mpaka walazimishwe.
Embu mpendwa tamani Leo kuwa Na Tabia kama ya Abramu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni