[1/6, 14:51] JHC: Shalom Mpendwa hongera Kwa Ibada Na karibu tena Kwenye Faragha hii tusome Neno La Mungu Kwa Pamoja Leo tutasoma Kitabu cha Mwanzo sura ya 5 mpaka sura ya 8.
Usiache kusoma.
Tuanze Na Kumkaribisha Roho Mtakatifu.
Fuatiliza sala hii:
"Nakushukuru Ee Mungu Baba, Mwana Na Roho Mtakatifu kwakuwa umetulinda Na kutufikisha Siku ya Leo. Ee Roho Mtakatifu naomba uongozi wako ninaposoma Neno hili LA Mwanzo 5-8. Macho yangu yatiwe nuru nione Na nisikie sauti yako katika neno hill. Ni katika Jina LA Yesu Kristo nimeomba amen. πππΌ
[1/6, 15:16] JHC: 1 Hiki ndicho kitabu cha vizazi vya Adamu. Siku ile Mungu alipoumba mtu, kwa sura ya Mungu alimfanya;
2 mwanamume na mwanamke aliwaumba, akawabariki akawaita jina lao Adamu, siku ile walipoumbwa.
3 Adamu akaishi miaka mia na thelathini, akazaa mwana kwa sura yake, kwa mfano wake, akamwita jina lake Sethi.
4 Siku za Adamu baada ya kumzaa Sethi zilikuwa miaka mia nane, akazaa wana, waume na wake.
5 Siku zote za Adamu alizoishi ni miaka mia kenda na thelathini, naye akafa.
6 Sethi akaishi miaka mia na mitano, akamzaa Enoshi.
7 Sethi akaishi baada ya kumzaa Enoshi miaka mia nane na saba, akazaa wana, waume na wake.
8 Siku zote za Sethi ni miaka mia kenda na kumi na miwili, akafa.
9 Enoshi akaishi miaka tisini, akamzaa Kenani.
10 Enoshi akaishi baada ya kumzaa Kenani miaka mia nane na kumi na mitano, akazaa wana, waume na wake.
11 Siku zote za Enoshi ni miaka mia kenda na mitano, akafa.
12 Kenani akaishi miaka sabini, akamzaa Mahalaleli.
13 Kenani akaishi baada ya kumzaa Mahalaleli miaka mia nane na arobaini, akazaa wana, waume na wake.
14 Siku zote za Kenani ni miaka mia kenda na kumi, akafa.
15 Mahalaleli akaishi miaka sitini na mitano, akamzaa Yaredi.
16 Mahalaleli akaishi baada ya kumzaa Yaredi miaka mia nane na thelathini, akazaa wana, waume na wake.
17 Siku zote za Mahalaleli ni miaka mia nane na tisini na mitano, akafa.
18 Yaredi akaishi miaka mia na sitini na miwili, akamzaa Henoko.
19 Yaredi akaishi baada ya kumzaa Henoko miaka mia nane, akazaa wana, waume na wake.
20 Siku zote za Yaredi ni miaka mia kenda na sitini na miwili, akafa.
21 Henoko akaishi miaka sitini na mitano, akamzaa Methusela.
22 Henoko akaenda pamoja na Mungu baada ya kumzaa Methusela miaka mia tatu, akazaa wana, waume na wake.
23 Siku zote za Henoko ni miaka mia tatu na sitini na mitano.
24 Henoko akaenda pamoja na Mungu, naye akatoweka, maana Mungu alimtwaa.
25 Methusela akaishi miaka mia na themanini na saba, akamzaa Lameki.
26 Methusela akaishi baada ya kumzaa Lameki miaka mia saba na themanini na miwili, akazaa wana, waume na wake.
27 Siku zote za Methusela ni miaka mia kenda na sitini na kenda, akafa.
28 Lameki akaishi miaka mia na themanini na miwili, akazaa mwana.
29 Akamwita jina lake Nuhu, akinena, Huyu ndiye atakayetufariji kwa kazi yetu na kwa taabu ya mikono yetu katika nchi aliyoilaani BWANA.
30 Lameki akaishi baada ya kumzaa Nuhu miaka mia na tisini na mitano, akazaa wana, waume na wake.
31 Siku zote za Lameki ni miaka mia saba na sabini na saba, akafa.
32 Nuhu alikuwa mwenye miaka mia tano, Nuhu akawazaa Shemu, na Hamu, na Yafethi.
'Mwanzo 5:1-2-3-4-5-6-7-8-9-10-11-12-13-14-15-16-17-18-19-20-21-22-23-24-25-26-27-28-29-30-31-32'
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.nippt.swahili.bible.free&hl=en
[1/6, 15:20] JHC: Katika Sura hii tunaona kizazi cha Adamu.
=> baada ya Kaini kumwua Habili. Mungu akamjalia Adamu mtoto mwengine ambaye Kwa Huyo ndipo baraka za Mungu ziliambatana naye.
Hapa tunajifunza kitu: Kaini alitenda dhambi Na kizazi chake chote watoto hadi wajukuu waliingia kwenye laana. Dhambi ni aibu ya watu wowoteπ♂
[1/6, 15:46] JHC: Pia Tunamwona HENOKO ambaye aliishi miaka 365 Na kwakuwa alikuwa mcha Mungu. Mungu alimpa Neema ya kutoonja Mauti. Huyu ni Mwanadamu Wa Kwanza kunyakuliwa Na Mungu
[1/6, 17:22] JHC: , *KITABU CHA MWANZO SURA YA SITA*
1 Ikawa wanadamu walipoanza kuzidi usoni pa nchi na wana wa kike walizaliwa kwao,
2 wana wa Mungu waliwaona hao binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wo wote waliowachagua.
3 BWANA akasema, Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye naye ni nyama; basi siku zake zitakuwa miaka mia na ishirini.
4 Nao Wanefili walikuwako duniani siku zile; tena, baada ya hayo, wana wa Mungu walipoingia kwa binti za wanadamu, wakazaa nao wana; hao ndio waliokuwa watu hodari zamani, watu wenye sifa.
5 BWANA akaona ya kuwa maovu ya mwanadamu ni makubwa duniani na kwamba kila kusudi analowaza moyoni mwake ni baya tu sikuzote.
6 BWANA akaghairi kwa kuwa amemfanya mwanadamu duniani, akahuzunika moyo.
7 BWANA akasema, Nitamfutilia mbali mwanadamu niliyemwumba usoni pa nchi; mwanadamu na mnyama, na kitambaacho na ndege wa angani; kwa maana naghairi ya kwamba nimewafanya.
8 Lakini Nuhu akapata neema machoni pa BWANA.
9 Hivi ndivyo vizazi vya Nuhu. Nuhu alikuwa mtu wa haki, mkamilifu katika vizazi vyake; Nuhu alikwenda pamoja na Mungu.
10 Nuhu akazaa wana watatu wa kiume, Shemu, na Hamu, na Yafethi.
11 Dunia ikaharibika mbele za Mungu, dunia ikajaa dhuluma.
12 Mungu akaiona dunia, na tazama, imeharibika; maana kila mwenye mwili amejiharibia njia yake duniani.
13 Mungu akamwambia Nuhu, Mwisho wa kila mwenye mwili umekuja mbele zangu; kwa sababu wameijaza dunia dhuluma, basi nitawaharibu pamoja na dunia.
14 Ujifanyie safina ya mti wa mvinje; fanya na vyumba ndani ya safina, ukaifunike ndani na nje kwa lami.
15 Hivi ndivyo utakavyoifanya; mikono mia tatu urefu wa safina, mikono hamsini upana wake, na mikono thelathini kwenda juu kwake.
16 Uifanyie safina mwangaza, ukaumalize juu kiasi cha mkono mmoja; ukautie mlango wa safina katika ubavu wake; ukaifanyie dari tatu, ya chini, ya pili, na ya tatu.
17 Na tazama, nitaleta gharika ya maji juu ya nchi, niharibu kila kitu chenye mwili na pumzi ya uhai, kisiwepo chini ya mbingu; kila kilichoko duniani kitakufa.
18 Lakini nitafanya agano langu nawe kuwa thabiti; nawe utaingia katika safina, wewe, na wanao, na mkeo, na wake za wanao, pamoja nawe.
19 Na katika kila kilicho hai chenye mwili, wawili wa kila namna utawaleta ndani ya safina, kuwahifadhi pamoja nawe; wawe mume na mke.
20 Katika vyote virukavyo kwa jinsi yake, na kila namna ya mnyama kwa jinsi yake, kila kitambaacho juu ya nchi kwa jinsi yake, wawili wa kila namna watakuja kwako ili uwahifadhi.
21 Ukajitwalie chakula cha kila namna kinacholika, ukakusanye, nacho kitakuwa ni chakula chenu na chao.
22 Ndivyo alivyofanya Nuhu, sawasawa na vyote alivyomwamuru Mungu, hivyo ndivyo alivyofanya.
[1/6, 17:35] JHC: Sura hii ya Sita tunaona habari za Nuhu Na Safina.
Mambo machache kama sio mawili tuu tuyatazame hapa Kwa upekee.
1. Mungu hukasirishwa Na maovu ya mwanadamu (soma mstar.6) Bwana anahudhunika moyo akiona jinsi tunavyomwasi.
-uovu huleta maangamizi.
_Mungu alighadhibika Na kutaka kufutilia mbali umbaji wake kwasababu tu ya makosa ya Mwanadamu. Tambua Mwanadamu kwamba wewe ni Wa Muhimu sana_
2. Kwasababu ya MTU mmoja NUHU Aliyekuwa mwema Na mcha Mungu, familia Na baadhi ya viumbe wachache waliokoka katika ghadhabu ya Mungu. Na hawa wakawa mbegu ya kuanzisha kizazi kipya/ulimwengu mpya.
Tambua mpendwa - Hata kama kwenye familia yako hawamchi Mungu wewe mmoja unatosha kwaajili ya ukombozi. Usikate tamaa endelea kumtumainia Mungu.
Mungu akubariki mpendwa wangu unayeendelea kufuatilia Kwa ukaribu sana
[1/6, 18:24] JHC: ππΌ *KITABU CHA MWANZO SURA YA SABA*
πππΌ
1 BWANA akamwambia Nuhu, Ingia wewe na jamaa yako yote katika safina; kwa maana nimekuona wewe u mwenye haki mbele zangu katika kizazi hiki.
2 Katika wanyama wote walio safi ujitwalie saba saba, mume na mke; na katika wanyama wasio safi wawili wawili, mume na mke.
3 Tena katika ndege wa angani saba saba, mume na mke; ili kuhifadhi hai mbegu juu ya uso wa nchi yote.
4 Kwa maana baada ya siku saba nitainyeshea dunia mvua, siku arobaini mchana na usiku; na kila kilicho hai nilichokifanya juu ya uso wa nchi nitakifutilia mbali.
5 Nuhu akafanya kama vile BWANA alivyomwamuru.
6 Naye Nuhu alikuwa mtu wa miaka mia sita hapo hiyo gharika ya maji ilipokuwa juu ya nchi.
7 Nuhu akaingia katika safina, yeye, na wanawe, na mkewe, na wake za wanawe pamoja naye; kwa sababu ya maji ya gharika.
8 Na katika wanyama walio safi, na wanyama wasio safi, na ndege, navyo vyote vitambaavyo juu ya nchi,
9 wakaingia katika safina alimo Nuhu, wawili wawili, mume na mke, kama vile Mungu alivyomwamuru Nuhu.
10 Ikawa baada ya siku hizo saba, maji ya gharika yakawa juu ya nchi.
11 Katika mwaka wa mia sita wa maisha ya Nuhu, mwezi wa pili, siku ya kumi na saba ya mwezi, siku ile chemchemi zote za vilindi vikuu zilibubujika kwa nguvu, madirisha ya mbinguni yakafunguka.
12 Mvua ikanyesha juu ya nchi, siku arobaini mchana na usiku.
13 Siku ile ile Nuhu akaingia katika safina, yeye, na Shemu na Hamu na Yafethi, wana wa Nuhu, na mkewe Nuhu, na wake watatu wa wanawe pamoja naye;
14 wao na kila mnyama wa mwitu kwa jinsi yake, na kila mnyama wa kufugwa kwa jinsi yake, na kila kitambaacho, chenye kutambaa juu ya nchi, kwa jinsi yake, na kirukacho kwa jinsi yake, kila ndege wa namna yo yote.
15 Waliingia katika safina alimo Nuhu, wawili wawili, wa kila chenye mwili kilicho na pumzi ya uhai ndani yake.
16 Na walioingia, waliingia mume na mke, wa kila kitu chenye mwili, kama vile alivyomwamuru Mungu; BWANA akamfungia.
17 Ile gharika ilikuwako juu ya nchi siku arobaini; nayo maji yakazidi, yakaieleza safina, ikaelea juu ya nchi.
18 Maji yakapata nguvu, yakazidi sana juu ya nchi; na ile safina ikaelea juu ya uso wa maji.
19 Maji yakapata nguvu sana sana juu ya nchi; na milima mirefu yote iliyokuwako chini ya mbingu ikafunikizwa.
20 Maji yakapata nguvu, hata ikafunikwa milima kiasi cha mikono kumi na mitano.
21 Wakafa wote wenye mwili waendao juu ya nchi, na ndege, na wanyama wa kufugwa, na kila mnyama wa mwitu, na kila kitambaacho chenye kutambaa juu ya nchi, na kila mwanadamu;
22 kila kitu chenye pumzi ya roho ya uhai puani mwake kikafa, kila kilichokuwako katika nchi kavu.
23 Kila kilicho hai juu ya uso wa nchi kikafutiliwa mbali tangu mwanadamu hata mnyama wa kufugwa, na kitambaacho, na ndege wa angani; vilifutiliwa mbali katika nchi, akabaki Nuhu tu, na hao walio pamoja naye katika safina.
24 Maji yakapata nguvu juu ya nchi siku mia na hamsini.
©JHC 2019
[1/6, 20:57] JHC: *KITABU CHA MWANZO SURA YA NANE*
✍ππ♂
1 Na Mungu akamkumbuka Nuhu, na kila kilicho hai, na wanyama wote waliokuwamo pamoja naye katika safina; Mungu akavumisha upepo juu ya nchi, maji yakapungua;
2 chemchemi za vilindi zikafungwa, pia na madirisha ya mbinguni, mvua kutoka mbinguni ikazuiliwa;
3 maji yakadumu kuondoka katika nchi; na mwisho wa siku mia na hamsini maji yakapunguka.
4 Mwezi wa saba, siku ya kumi na saba ya mwezi, safina ikatua juu ya milima ya Ararati.
5 Maji yakapunguka-punguka hata mwezi wa kumi; mwezi huo wa kumi, siku ya kwanza ya mwezi, vilele vya milima vikaonekana.
6 Ikawa baada ya siku arobaini, Nuhu akalifungua dirisha la safina, alilolifanya;
7 akatoa kunguru, naye akatoka akaenda huko na huko, hata maji yakakauka juu ya nchi.
8 Kisha akatoa njiwa, aone kwamba maji yamepunguka usoni pa nchi;
9 bali yule njiwa hakuona mahali pa kutua kwa wayo wa mguu wake, akamrudia Nuhu safinani, maana maji yalikuwa juu ya uso wa nchi yote; naye akanyosha mkono, akamtwaa, akamwingiza mle safinani.
10 Akangoja na siku saba tena; kisha akamtoa yule njiwa katika safina mara ya pili,
11 njiwa akamjia jioni, na tazama, alikuwa na jani bichi la mzeituni kinywani mwake, ambalo amelitunda, basi Nuhu akajua ya kwamba maji yamepunguka juu ya nchi.
12 Akangoja na siku saba tena, akamtoa yule njiwa; naye asimrudie tena kamwe.
13 Ikawa mwaka wa mia sita na moja, mwezi wa kwanza, siku ya kwanza ya mwezi, maji yalikauka juu ya nchi. Nuhu akaondoa kifuniko cha safina, naye akaona, na tazama, uso wa nchi umekauka.
14 Na mwezi wa pili, siku ya ishirini na saba ya mwezi, nchi ilikuwa kavu.
15 Mungu akamwambia Nuhu, akisema,
16 Toka katika safina, wewe, na mkeo, na wanao, na wake za wanao pamoja nawe.
17 Utoe pamoja nawe kila kilicho hai kilichomo pamoja nawe, chenye mwili, ndege, na mnyama, na kila kitambaacho, chenye kutambaa juu ya nchi; wajae katika nchi, wawe na uzazi, wakaongezeke katika nchi.
18 Basi Nuhu akatoka, yeye, na wanawe, na mkewe, na wake za wanawe pamoja naye;
19 kila mnyama, na kila kitambaacho, na kila ndege, kila kinachokwenda juu ya nchi kwa kabila zao, wakatoka katika safina.
20 Nuhu akamjengea BWANA madhabahu; akatwaa katika kila mnyama aliye safi, na katika kila ndege aliye safi, akavitoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu.
21 BWANA akasikia harufu ya kumridhisha; BWANA akasema moyoni, Sitailaani nchi tena baada ya hayo kwa sababu ya wanadamu, maana mawazo ya moyo wa mwanadamu ni mabaya tangu ujana wake; wala sitapiga tena baada ya hayo kila kilicho hai kama nilivyofanya.
22 Muda nchi idumupo, majira ya kupanda, na mavuno, wakati wa baridi na wakati wa hari, wakati wa kaskazi na wakati wa kusi, mchana na usiku, havitakoma.
'Mwanzo 8:1-2-3-4-5-6-7-8-9-10-11-12-13-14-15-16-17-18-19-20-21-22'
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.nippt.swahili.bible.free&hl=en
©2019 JHC READING BIBLE CAMPAINGπππ
[1/6, 21:04] JHC: Tunajifunza Mengi katika Sura hii ila machache ninayotaka kuya highlight ni Haya:
1. WOKOVU NI WA MMOJA SIO KUNDI. Mungu anaangalia moyo unaohitaji kukombolewa Na anaandaa njia ya kuuokoa Hata mbele za adui zako.
2. Hata katikati ya ghadhabu Yake ameandaa sehemu salama ya Wale wote wanaomcha Na kuzitii amri zake. NUHU alikuwa salama humu humu duniani ndani ya Safina wakati Dunia inaharibiwa yote.
3. Safina Yetu ni Yesu Kristo. Tukiingia ndani Yake tupo salama hata paje kitu gani kiwezacho kuzuru/ kuharibu ulimwengu wote lakini ndani ya Kristo tupo salama. Hata ije mauti iwezayo kuuangamiza mwili huu lakini walio Katika Kristo wataishi milele.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni